Breaking News

Profesa Lipumba, Kauli ya Rais Magufuli Kuwa Uchaguzi Utakuwa Uhuru na Haki Inatia Faraja

Chama cha wananchi CUF kimesema kimefarijika na kauli ya Rais John Magufuli kuhusu kuhakikisha uchaguzi mkuu wa mwaka huu utafanyika huru na haki.

Akizungumza makao makuu ya chama jijini Dar es salaam Mwenyekiti wa chama hicho Profesa Ibrahim Lipumba alisema kauli hiyo kama itatekelezwa na kusimamiwa vizuri itasaidia kujenga na kutekeleza Amani, Umoja na utulivu uliopo nchini.

Alisema kama chama wanaamini rais hayupo tayari kuiingiza nchi kwenye machafuko kama uchaguzi autakuwa huru na wa haki.

"Cuf ina amini kuwa kauli ya rais Magufuli kwa kuzingatia ameitoa mbele ya wanadiplomasia ambao ni mabalozi wanaowakilisha nchi zao nchini inaonyesha wapi ana dhamila ya kweli kuhakikisha uchaguzi ujao utakuwa huru na haki" alisema Profesa Lipumba.

Profesa Lipumba aliongeza kuwa pamoja na kauli hiyo yenye kutia faraja ametoa wito kwa Rais Magufuli kuhakikisha natembea na kutekeleza kwa vitendo kauli yake hiyo kwa mustakabadhi wa taifa.

Alisema uchaguzi huru na wa haki ni zao la mchakato na sio tukio la siku moja, hivyo kusisitiza uandaaji wa mazingira ambayo yatapelekea uchaguzi huo kuwa uhru na haki.

Ametaja maeneo ambayo chama hicho inaona yanahitaji kufanyiwa marekebisho ni pamoja na kuondolewa kwa zuio la mikutano ya hadhara ya vyama vya upinzani kuwezesha vyama vyote kushiriki kufikisha itikadi na sera zao kwa wananchi.

Lingine ni kumwomba rais Magufuli kuangalia uwezekano wa kukutana na viongozi wa vyama vya siasa kubadilishana nao mawazo ikiwemo namna bora ya kuboresha tume ya uchaguzi kwa lengo la kusimamia uchaguzi uwe huru na haki kwa ufanisi.

Profesa Lipumba ametoa rai kwa wana Cuf wote nchini kutambua kuwa mchakato wa kudai na kujenga demokrasia utafanikiwa kwa wao kushiriki mchakato mzima wa kuidai Demokrasia hata kama mazingira ni magumu.