Breaking News

Maalimu Seif Atangaza Maazio ya Mkutano Mkuu Taifa wa Pili wa ACT Wazalendo

Chama cha ACT Wazalendo kilifanya Mkutano Mkuu Taifa wa Pili katika ukumbi wa Mlimani City, Dar es salaam. Ambapo Chama chetu umethibitisha nguvu ya Chama kimtandao na uendeshaji wa mambo.

Katika siku mbili za mkutano, Wajumbe wa Mkutano Mkuu walifanya maamuzi na kufikia maazimio mbalimbali yanayogusa uendeshaji wa Chama chetu na siasa za nchi yetu. Maazimio makuu ya Mkutano Mkuu Taifa wa Pili wa Chama cha ACT Wazalendo yalikuwa kama ifuatavyo;

1. Maboresho ya Katiba ya Chama.

Kwa kauli moja, wajumbe wa Mkutano Mkuu waliridhia maboresho ya katiba ya ACT Wazalendo ili kuongeza ufanisi na kuimarisha Chama. Maboresho haya ya Katiba yanalenga pia kutekeleza matakwa ya Sheria ya Vyama vya Siasa ya Mwaka 2019 ambayo pamoja na mambo mengine yanavitaka vyama vya siasa kurekebisha katiba zake ili kuendana na sheria hiyo. 

Maboresho ya katiba ya ACT Wazalendo, pamoja na mambo mengine yamezingatia usawa wa kijinsia na uwiano wa pande mbili za muungano. 

*2. Hesabu za Chama za Miaka Mitano.*

Mkutano Mkuu Taifa ulipitia na kupitisha hesabu za ACT Wazalendo kwa kipindi cha miaka mitano iliyopita (2015-2020). Mkutano Mkuu ulisisitiza juu ya haja ya Chama cha ACT Wazalendo kuendeleza utamaduni wake wa uwazi (transparency) katika usimamizi na matumizi ya fedha za Chama.

*3. Uchaguzi wa Viongozi Wakuu wa Kitaifa.*

Mkutano Mkuu ulichagua viongozi Wakuu wa Chama ambao kwa mujibu wa Katiba, wanapaswa kuchaguliwa. Viongozi waliochaguliwa ni; 

*Zitto Kabwe (Kiongozi wa Chama),*

*Maalim Seif Sharif Hamad (Mwenyekiti Taifa),*

*Dorothy Semu (Makamu Mwenyekiti Bara) na*

*Juma Duni Haji (Makamu Mwenyekiti Zanzibar).*

Halmashauri Kuu iliwachagua pia wajumbe wa Halmashauri Kuu, chombo cha pili kwa ukubwa baada ya Mkutano Mkuu. Ni jambo linalotia moyo kuwa, kati ya wajumbe 15 wa Halmashauri Kuu waliochaguliwa, 8 ni wanawake ambao ni sawa na 53%. Hata kwa wajumbe wa Kamati Kuu ambao jana wamechaguliwa na Halmashauri Kuu, kati ya wajumbe 8, wajumbe 4 ni wanawake sawa na 50%.

Bodi ya Wadhamini ya Chama chetu, chombo kikuu cha kusimamia Fedha za Chama kina uwakilishi mkubwa wa wanawake kuliko wanaume. Kati ya wajumbe 9 wa Bodi ya Wadhamini, 5 ni wanawake sawa na 55%.
Kwa hakika, ACT Wazalendo kimethibitisha kuwa ni Chama kinachojali usawa wa kijinsia kwa vitendo kwa kuwachagua na kuwateua wanawake kwenye vyombo muhimu vya kimaamuzi na nafasi mbalimbali za kimkakati. 

Vijana pia, wamepata nafasi ya kipekee kwenye nafasi na vyombo mbalimbali vya kimaamuzi. ACT Wazalendo tunaamini kwamba vijana, baada ya kupata malezi ya kiuongozi wanastahili kuaminiwa kwa kupewa nafasi za kuonesha vipaji vyao.

*4. Ushirikiano na vyama vingine vya siasa.*

Mkutano Mkuu Taifa kwa kauli moja umeunga mkono ushirikiano wa Chama cha ACT Wazalendo na vyama vingine vya siasa katika uchaguzi na katika kuilinda na kuipigania Demokrasia. Mkutano Mkuu Taifa umeazimia kuwa Chama cha ACT Wazalendo kishirikiane na vyama vingine makini vya siasa na makundi mbalimbali ya kijamii kutekeleza Azimio la Zanzibar la Mwaka 2018 ambalo lilisisitiza juu ya kuundwa kwa mshikamano wa makundi mbalimbali ya kijamii (Grand Coalition) katika kupambana na udhalimu, dhulma na udikteta wa CCM.

*5. Tume Huru ya Uchaguzi.*

Mkutano Mkuu ulisisitiza juu ya ulazima wa Chama kushirikiana na wadau wengine wa Demokrasia kupigania Tume Huru ya Uchaguzi. Licha ya changamoto zilizopo katika mfumo mzima wa kusimamia chaguzi zetu, Mkutano Mkuu uliweka bayana kuwa Chama hakitasusia uchaguzi. Kwetu ACT Wazalendo huu ni uchaguzi muhimu sana.

Kwa upande wa Zanzibar, ni dhahiri kuwa CCM imeshafahamu kuwa haiwezi kushinda uchaguzi. ACT Wazalendo tumejipanga na kujizatiti kuhakikisha kuwa tunalinda ushindi wetu kwa gharama yoyote.

Kwa upande wa Tanzania Bara, Chama kimejipanga kuhakikisha tunashinda viti vingi zaidi vya Udiwani, Ubunge, kuongoza Halmashauri na kushirikiana na vyama vingine makini vya upinzani kuhakikisha CCM, chama kilichochoka, kinaondoka madarakani.

*Maalim Seif Sharif Hamad,*
*Mwenyekiti wa Chama Taifa,*
*ACT Wazalendo.*
*17 Machi  2020.*.

Tarehe 14 na 15 Machi 2020, Chama cha ACT Wazalendo kilifanya Mkutano Mkuu Taifa wa Pili katika ukumbi wa Mlimani City, Dar es salaam. Tunashukuru kwamba mkutano huo wa kihistoria ulioendeshwa kwa viwango vya hali ya juu ulifanyika kwa amani na kwa mafanikio makubwa. Bila shaka, kwa namna ulivyoandaliwa na kuendeshwa, Mkutano Mkuu wa Pili wa Chama chetu umethibitisha nguvu ya Chama kimtandao na uendeshaji wa mambo.

Katika siku mbili za mkutano, Wajumbe wa Mkutano Mkuu walifanya maamuzi na kufikia maazimio mbalimbali yanayogusa uendeshaji wa Chama chetu na siasa za nchi yetu. Maazimio makuu ya Mkutano Mkuu Taifa wa Pili wa Chama cha ACT Wazalendo yalikuwa kama ifuatavyo;

1. Maboresho ya Katiba ya Chama.

Kwa kauli moja, wajumbe wa Mkutano Mkuu waliridhia maboresho ya katiba ya ACT Wazalendo ili kuongeza ufanisi na kuimarisha Chama. Maboresho haya ya Katiba yanalenga pia kutekeleza matakwa ya Sheria ya Vyama vya Siasa ya Mwaka 2019 ambayo pamoja na mambo mengine yanavitaka vyama vya siasa kurekebisha katiba zake ili kuendana na sheria hiyo. 

Maboresho ya katiba ya ACT Wazalendo, pamoja na mambo mengine yamezingatia usawa wa kijinsia na uwiano wa pande mbili za muungano. 

2. Hesabu za Chama za Miaka Mitano.

Mkutano Mkuu Taifa ulipitia na kupitisha hesabu za ACT Wazalendo kwa kipindi cha miaka mitano iliyopita (2015-2020). Mkutano Mkuu ulisisitiza juu ya haja ya Chama cha ACT Wazalendo kuendeleza utamaduni wake wa uwazi (transparency) katika usimamizi na matumizi ya fedha za Chama.

3. Uchaguzi wa Viongozi Wakuu wa Kitaifa.

Mkutano Mkuu ulichagua viongozi Wakuu wa Chama ambao kwa mujibu wa Katiba, wanapaswa kuchaguliwa. Viongozi waliochaguliwa ni; 

Zitto Kabwe (Kiongozi wa Chama),

Maalim Seif Sharif Hamad (Mwenyekiti Taifa),

Dorothy Semu (Makamu Mwenyekiti Bara) na

Juma Duni Haji (Makamu Mwenyekiti Zanzibar).

Halmashauri Kuu iliwachagua pia wajumbe wa Halmashauri Kuu, chombo cha pili kwa ukubwa baada ya Mkutano Mkuu. Ni jambo linalotia moyo kuwa, kati ya wajumbe 15 wa Halmashauri Kuu waliochaguliwa, 8 ni wanawake ambao ni sawa na 53%. Hata kwa wajumbe wa Kamati Kuu ambao jana wamechaguliwa na Halmashauri Kuu, kati ya wajumbe 8, wajumbe 4 ni wanawake sawa na 50%.

Bodi ya Wadhamini ya Chama chetu, chombo kikuu cha kusimamia Fedha za Chama kina uwakilishi mkubwa wa wanawake kuliko wanaume. Kati ya wajumbe 9 wa Bodi ya Wadhamini, 5 ni wanawake sawa na 55%.
Kwa hakika, ACT Wazalendo kimethibitisha kuwa ni Chama kinachojali usawa wa kijinsia kwa vitendo kwa kuwachagua na kuwateua wanawake kwenye vyombo muhimu vya kimaamuzi na nafasi mbalimbali za kimkakati. 

Vijana pia, wamepata nafasi ya kipekee kwenye nafasi na vyombo mbalimbali vya kimaamuzi. ACT Wazalendo tunaamini kwamba vijana, baada ya kupata malezi ya kiuongozi wanastahili kuaminiwa kwa kupewa nafasi za kuonesha vipaji vyao.

4. Ushirikiano na vyama vingine vya siasa.

Mkutano Mkuu Taifa kwa kauli moja umeunga mkono ushirikiano wa Chama cha ACT Wazalendo na vyama vingine vya siasa katika uchaguzi na katika kuilinda na kuipigania Demokrasia. Mkutano Mkuu Taifa umeazimia kuwa Chama cha ACT Wazalendo kishirikiane na vyama vingine makini vya siasa na makundi mbalimbali ya kijamii kutekeleza Azimio la Zanzibar la Mwaka 2018 ambalo lilisisitiza juu ya kuundwa kwa mshikamano wa makundi mbalimbali ya kijamii (Grand Coalition) katika kupambana na udhalimu, dhulma na udikteta wa CCM.

5. Tume Huru ya Uchaguzi.
Mkutano Mkuu ulisisitiza juu ya ulazima wa Chama kushirikiana na wadau wengine wa Demokrasia kupigania Tume Huru ya Uchaguzi. Licha ya changamoto zilizopo katika mfumo mzima wa kusimamia chaguzi zetu, Mkutano Mkuu uliweka bayana kuwa Chama hakitasusia uchaguzi. Kwetu ACT Wazalendo huu ni uchaguzi muhimu sana.

Kwa upande wa Zanzibar, ni dhahiri kuwa CCM imeshafahamu kuwa haiwezi kushinda uchaguzi. ACT Wazalendo tumejipanga na kujizatiti kuhakikisha kuwa tunalinda ushindi wetu kwa gharama yoyote.

Kwa upande wa Tanzania Bara, Chama kimejipanga kuhakikisha tunashinda viti vingi zaidi vya Udiwani, Ubunge, kuongoza Halmashauri na kushirikiana na vyama vingine makini vya upinzani kuhakikisha CCM, chama kilichochoka, kinaondoka madarakani.

Maalim Seif Sharif Hamad,
Mwenyekiti wa Chama Taifa,
ACT Wazalendo.
17 Machi  2020.