NCCR Mageuzi Yasitisha Mikutano Yake Yote Kutokana na Corona

Chama cha Nccr Mageuzi kimetangaza kusitisha mikutano yake yote ya hadhara kufatiwa kuripotiwa na serikali tayali kirusi kinacho sababisha ugonjwa wa Corona kuingia nchini.
Akitoa uamuzi huo jijini Dar es salaam, Mwenyekiti wa chama hicho mhe. Jemsi Mbatia alisema uuzi huo ni jitihada za chama hicho kuhakikisha kirusi hicho hakisambai zaidi nchinj.
"Chama kimeamua kusiyisha mikutano na mikusanyiko yote ambayo ilikuwa ifanyike ktokana na kuripotiwa kuwepo kwa kirusi cha ugonjwa wa Corona nchini na kutambua ushauri ambao umetolewa na wataalam kuzuia kusambaa kwa kirusi hizo hivyo chama kimeamua kusitisha" Alisema mhe Mbatia.
Alisema Kutokana na taadhari ambazo zimetolewa na seriklai kupitia wizara ya afya na shirika la afya Dunian WHO juu ya kirusi hiki na namna ambavyo kimekua kikisambaa kwa kasi duniani chama kimuamua kuchukua uamuzi huo.
Mhe mbatia aliongeza kuwa mamlaka husika kutoa taarifa sahihi na kwa wakati juu ya wagonjwa popote kwan mpka sasa ugonjwa huo auna kinga na tiba pekee ni kujikinga jukumu ambalo ni la kila mmoja wetu.



