Profesa Lipumba Hotuba ya Bajeti ya Waziri Mhuu, Aijagusia Kabisa Athari Zitakazojitokeza Kuhusu CORONA
Mwenyekiti wa chama cha wananchi CUF, Profesa Ibrahim Lipumba ameelezea kushitushwa kwake na serikali kushindwa kuonyesha msisitizo na mkazo wa janga la virusi vya COVID-19 na kitozingatia athari kubwa zinazoweza kutokea ikiwa maradhi haya yatasambaa zaidi.
Akizungumza jijini Dar es salaam alisema chama cha wananchi CUF kinaunga mkono hatua ambazo zimekuwa zikichukuliwa na serikali kupambana na janga hili nchini ila cha kusikitisha katika hotuba ya bajeti ya waziri mkuu haizingatii athari ambazzo zinaweza kutokea kwa kusambaa ugonjwa huo.
"Cuf imekuwa ikiunga mkono jitihada ambazo zimekuwa zikichukuliwa na serikali kupambana na ugonjwa wa COVID-19 ila tumesikitika sana mara baada ya kusomwa kwa hotuba ya bajeti ya waziri mkuu ambayo ukiondoa maelezo ya awali jinsi serikali imejipanga hotuba hii bado haizongatii athari zinazoweza jitokeza pindi utakapo sambaa ugonjwa huu" Alisema Prof. Lipumba.
Alisema mhe waziri mkuu ajaeleza hatua za kibajeti zilizochukuliwa zaidi ya kupeleka fedha za mbio za mwenge kukabiliana na COVID-19 wakati taarifa za wataalam wa afya zinasema kuwa jitihada zaidi zinatakiwa kuongezwa katika upimaji wa wananchi wanaodhaniwa kuwa na maambukizi ya virusi hivyo na wasiokuwa na dalili za maambukizi.
"Mkakati wa kuzuia kuenea maambukizi ya virusi vya Corona ni kupima na kuwakarantini wale wote wanaoingia nchini na wanahoisiwa kuwa na dalili za ugonjwa huo kwa muda wa siku 14 hasa katika miji inayopokea wageni wengi Dar es salaam, Arusha, Zanzibar na Mwanza" Alisema
Aidha Prof Lipumba aliongeza kuwa kwa mujibu wa taarifa ya hali ya maambukizi ya ugonjwa huo nchini kuwa ni 20 huu ndio wakati muafaka wa kudhibiti mnyororo wa wa maambukizi kwa hatua pana na kwa kasi ikiwemo kuongeza upimaji, kuongeza mahabara za kupimia pamoja na kuwa na mkakati wa dharura wa kukabiliana na maambukizi kama likitokea.




