Mgombea Udiwani Jangwani CHADEMA Atoa Ufafanuzi Juu ya Sakata la Kuenguliwa Kwake

Mgombea wa udiwani kata ya Jangwani CHADEMA ametolea ufafanuzi sintofahamu iliyopo juu ya hatma yake juu ya ushiriki wake wa uchaguzi kufatia kuenguliwa kimizengwe kugombea nafasi hiyo katika ambao unataraji kufuanyika nchi nzima octoba 28.
Akizungumzia sakata hilo mapema leo jijini Dar es salaam mgombea huyo kupitia chama cha demokrasia na maendeleo CHADEMA, bw. Furaha mbakile alisema mpaka mda huu haifahamiki kinacho endelea kuhusu hatma ya rufaa yake kufatia kuandika barua ya kujibu pingamizi alilowekewa kimizengwe na kinyume na kuenguliwa.
"Kwasasa naona hakuna tena dalili ya kutendeka kwa haki baada ya kugundua hata barua rufaa yangu ya kujibu pingamizi aikwenda kwa wakati"
Pamoja na kuwepo na dosari za wazi katika hatua ya awali kabisa za kuondolewa kwake kama vile msaidizi wa uchaguzi kumwengua ambapo kisheria astahili kufanya hivyo bila kumshirikisha msimamizi wa uchaguzi.
Kufatia sintofahamu hii niwaombe wote ambao wanahusika na jambo hili kulipatia ufumbuzi wa haraka kwa lengo la kuwapa fursa wananchi kuchagua mgombeaa wanaemtaka kuliko huu uhuni unaoendelea.
"Nitoe wito wahusika wa sakata hili hususani msimamizi wa uchaguzi kulipatia ufumbuzi na wagombea tuende kunadi sera zetu ili wananchi wachague mgombea wanaeona anafaa iwe wa CUF, ATC Wazalendo, Ccm au Chadema kuliko huu uhuni unaoendelea" Alisema bw Mbakile.



