Waziri JAFO Mgeni Rasmi Tuzo za Wahitimu Waliofanya Vizuri Kidato Nne na Sita Mwaka 2019/20 Jijini Dar.
waziri was Tamisemi mhe. Suleiman Jafo anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika hafla ya lutoa Tuzo kwa wanafunzi waliofanya vizuri katika mitihani ya kuhitimu masomobyao ya kidato cha NNE mwaka 2019 na kidato cha sita mwaka 2020 zitakazotolewa kesho katika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es salaam.
Akizingumza jijini Dar es salaam katibu mtendaji wa baraza la mtihani nchini Dkt. Charles Msonde alisema tuzo hizo wahitimu waliomaliza na kufanya vizuri katika mitihani yao ya mwisho ya kidato cha NNE na kidato cha sita nchi nzima watatunukiwa tuzo hizo.
"Tuzo hizi mahususi kwa ajili ya kuwatunuku wahitimu walifanya vizuri masomo kwa wanafunzi was kidacho cha NNE na sita pamoja na walimu nchi nzima"
Alisema baraza la mitihani tayali limekamilisha jukumu la kuchambua, kuwatambua na kuwasilisha majina ya wanaostahili nchi nzima ambao wanakidhi vigezo vya kutunukiwa tuzo hizo" Alisema dkt. Msonde.
Tuzo hizo ambazo ambazo zimeanzishwa mahususi kutoa motisha kwa wanafunzi na walimu kujituma zaidi zimeandaliwa na shirika la Global International link kwa kushirikiana na wizara ya Tamisemi zinatarajo kuwashirikish azaidi ya wahitimu 200 kutoka nchi nzima.



