ACT WAZALENDO YAANIKA MIKAKATI YAKE KUELEKEA UCHAGUZI 2025
Na Timothy Marko
Chama cha Act wazalendo kimesema kinatarajiakuendesha Chama hicho kijiditali ambapo wanachama wake wanaweza kujisajili kupitia App mpya Act kiganjani.
Akizungumza katika mkutano wa waandishi Habari jijini Dar es Salaam Mwenyekiti wa Chama hicho mhe. Juma Haji Duni amesema moja ya ajenda watakazotilia mkazo kuelekea uchaguzi mkuu wa 2025 ni mapambano ya katiba mpya na tume huru ya uchaguzi.
"2022 ACT wazalendo tumelenga kupigania tume huru ya uchaguzi, na kujipambanua kisiasa".Alisema Mwenyekiti Duni Haji .
Mwenyekiti Duni alisema katika Mwaka 2022 Chama hicho kimelenga kutekeleza malengo yake katika kuimarisha ikiwemo kuimarisha Haki na Maridhiano katika Chama hicho.
Aliongeza kuwa ajenda zingine ni Mwaka 2022 wa kuimarisha haki Sawa Zanzibar na Tanzania bara.
Kwa upande wake Makamu Mwenyekiti wa Chama hicho Zanzibar, mhe Othuman Masudi alisema Chama kimeweka nguvu kubwa katika visiwa vya Zanzibar Kwa sababu zaidi ya Asilimia 60 ya wanachama wake wanapatikana Zanzibar.
Alisema katika Siasa za Zanzibar kuna badhi ya mambo yanatakiwa kurekebishwa ikiwemo wahanga wa uchaguzi na huduma za afya.
"Zanzibar kuna Mambo inabidi yafanyiwe marekebisho hususani katika Jimbo la konde". Alisema Othuman Masudi.



