Breaking News

WATUHUMIWA 17 WAKATWA KWA KUZALISHA NA KUUZA JEZI FEKI ZA TIMU YA YANGA

Na Timothy Marko
Jeshi la polisi kanda Maalum ya Dar es Salaam linawashikilia watuhumiwa 17 Kwa tuhuma za kuuza jezi feki za timu Yanga zaidi elfu moja mia mbili.

Akizungumza katika mkutano jijini Dar es Salaam Kamanda Jeshi la polisi  wa kanda Maalum ya Dar es Salaam, Jumanne Muliro  amesema katika operesheni iliyofanywa kuanzia January 2 hadi January 28 mwaka huu wamefanikiwa kuwakamata watuhumiwa hao wakiwa na jezi hizo.

Ametaja maeneo ambayo watuhumiwa hao wamekamatwa kuwa ni jiji la Dar es salaam ambapo jumla ya watuhumiwa watano wamekamatwa akiwemo bwana Zahiri Hassani (17) ambae amekamatwa katika uwanja wa Benjamin mkapa akiwa na jezi 52, Majiba Ndahya (50) ambae amekamatwa Kariakoo mtaa wa Agrey akiwa na jezi 124, Mohamed  Ramadhani (26) jezi 86, John Stanslaus (19) jezi 39 na Emmanuel Kinasa (21) jezi 60.

Kamanda muliro aliongeza kuwa mara baada ya kukamatwa watuhumiwa hao waliwahoji waliwataja wenzao wengne ambao baadhi yao tayali wanashikiliwa na kuongeza kuwa pia katika uwanja wa Amani Zanzibar watuhumiwa watatu walikutwa na jezi bandia 36, Mkoa wa Tanga na Mwanza watuhumiwa 9 walikutwa na jezi 811

Aidha jeshi la polisi kanda maalumu Dar es salaam linawatahadharisha wananchi wote wanaojihusisha na vitendo vya kutengeneza  kuuza na kusambaza bidhaa Kwa kuiga kufananisha nembo za Biashara au huduma za watu wengine iliyosajiliwa kisheria Kufanya hivyo ni kosa na kinyume na  sheria za Nchi.