ACT WAZALENDO YAWATAKA WANACHAMA WAKE KUPUUZA UVUMI BAADHI YA VIGOGO WAKE KUTAKA KUREJEA CUF
Chama cha ACT Wazalendo kimewataka wafuasi wake na wapenda mageuzi kupuuza taarifa ambazo zimekuwa zikisambaa katika mitandao ya kijamii kuwa baadhi ya vigogo wa chama hicho wako katika mpango wa kurejea katika chama chao cha zamani (CUF)
Akizungumza makao makuu ya chama jijini Dar es salaam, katibu wa Organization mafunzo taifa bw. Shaweji Mketo amesema taarifa hizo si za kweli zimesambazwa na wafuasi wa chama hicho kinachoitwa cha zamani kwa nia ovu kwa lengo kuleta sintofahamu kwa wanachama wa chama chetu.
"Kumekuwepo na uvumi hususani katika mitandao ya kijamii na baadhi ya vituo vya radio kuwa kuna kundi la vigogo na vingozi wengine waandamizi wa chama hicho wamepanga kurejea katika chama chao cha zamani CUF jambo ambalo si kweli"
Ametaka wanachama na wapenda mageuzi kupuuza uvumi huo kwani umetengenezwa na wafuasi wa chama hicho kinachoitwa cha zamani kwa lengo la kuleta taharuki kwa wafuasi wao kwani baadhi ya wanachama wamekuwa wakipiga simu watajwa kutaka kujua juu ya uvumi huo.
"Katika kipindi cha siku mbili zilizopita wanachama wa ACT kutoka bara na visiwani wamekuwa wakipiga simu kwa baadhi ya viongozi ambao wametajwa kutaka kurejea chama katika chama chao cha zamani kutaka kujua juu ya uvumi huo na kitu gani kimetokeabmpaka wamefikia maamuzi hayobila kujadiliana nao"
Bw Shaweji amewataka wafuasi wa chama cja ACT wazalendo kupuuza uzushi huo kwani wao awajawahi, hatutawahi wala hatowahi hata siku moja kifikilia kinachoitwa kurejea katika chama chao cha zamani kwani awana sababu ya kurejea huko na haitokuwepo kamwe.
Nae Kaimu katibu mkuu wa ACT mkoa wa Dar es salaam bw. Twaha Rashid alisema uamuzi wa kuama chama cha wanachi CUF wakiongozwa na mhe. Maalim Sif Sharif wa kuhamia chama cha ACT Wazalendo ulifanyika baada ya kufanyika utafiti makini kabla ya kufikiwa uamuzi huo.
"Ifahamike kuwa kabla ya kuhamia chama cha ACT ulifanyika utafiti wa kina na viongozi wote wakajikubaliana niwatoe hofu wanachama, wafuasi na wapenda mageuzi wote kupuuza uvumi huo kwani jambo hilo halitoweza tokea" Alisema bw. Rashid.
Alisema wanachama wetu wamekuwa wakipigiwa simu kushawishiwa na pia kuwepo na uvumi ukiusisha kutaja majina ya matawi makubwa ya chama ikiwapo tawi maarufu la kosovo kwa lengo la kuwaadaa wanachama wetu niwatoe hofu wanachama wetu kupuuza uvumi huo matawi hayo yapo salama yanaendelea na zoezi la kuandikisha wanachama kadi za kidijitali la ACT kiganjani.



