HAMAD MASOUD AREJEA RASMI CUF APOKELEWA NA KUKABIDHIWA KADI YA UANACHAMA NA PROF. LIPUMBA
Aliyekuwa mgombea wa nafasi ya Mwenyekiti kupitia chama cha ACT wazalendo iliyokuwa wazi kufatia kufariki aliyekuwa mwenyekiti wa chama hicho Maalim Seif Sharif mhe. Injinia Hamad Masoud Hamad amerejea rasmi na kujiunga na chama cha wananchi CUF
Akizungumza katika hafla ya kuwapokea ambapo ameambatana na wenyeviti wa mikoa na mamia ya wanachama wengine makao makuu ya chama cha CUF jijini Dar es salaam, Mwenyekiti wa CUF taifa Profesa Ibrahim Lipumba alisema amewakaribisha na kuwapongeza kwa uamuzi wao wa kuamua kurudi nyumbani hili kuendelea kujenga Chama hicho
Alisema wanachama na viongozi wa chama cha wananchi nchini kuendelea na zoezi la kuwakaribisha wanachama wote ambao wameamua kurejea pamoja na kuwashawishi wengine kujiunga na chama.
"Viongozi wa chama cha wananchi CUF, Bara na Zanzibar kutambua kuwa wanachama wanaorejea na kujiunga na chama hicho wanao wajibu wa kukilinda na kukijenga chama kwa mujibu wa katiba ya chama hivyo wapatiwe ushirikiano kwa kadri inavyowezekana ," Alisema Prof. Lipumba.
Alisema amewataka wanachama na viongozi wa chama hicho nchi nzima kuendelea na zoezi la kuwakaribisha wanachama wapya wanahitaji kujenga chama imara kitakachoweza kulinda na kuhakikisha rasilimali za nchi zinatumika kwa maslahi ya wananchi wote.
"Nitoe wito kwa wanachama na waasisi wa chama chetu kazi kubwa iliyo mbele yetu ni kukijenga chama katika misingi ya haki na usawa kwa wote hii itawezekana kama tutaweza kuanza kudai katiba mpya ambayo inatokana na maoni ya wananchi na Tume Huru ya Uchaguzi" Aliongeza Prof Lipumba
Nae Aliyekuwa Mwanachama wa chama cha ACT Wazalendo Injinia Hamad Masoud Hamad akizungumza mara baada ya kupokea kadi ya uanachama CUF amewashukuru vingozi wote na wanachama wa chama cha wananchi CUF kwa kukubali kuwapokea yeye na wenzake kwani ni faraja kwao kurejea nyumbani na kupokelewa vizuri.
Alisema ameamua kurejea nyumbani na wamefatijika sana kwa mapokezi walioyapata kutoka kwa viongozi na wanachama napenda kuwahaidi kuwa kwa kushirikiana na viongozi wenzangu na wanachama nitahakikisha nakirejesha chama katika hadhi yake hususani visiwani Zanzibar.
"Tuliikuta ACT Machi 18, 2019 ikiwa na ofisi mbili Zanzibar, lakini kufumba na kufumbua Machi 19, 2019 ikajikuta ina ofisi 614. Kwa uwezo wa Mwenyezi Mungu tukifanya kazi tutahakikisha ACT tunairudisha katika hadhi yake ya ofisi mbili au tatu," Alisema Hamad.
Aidha Injinia Hamad aliongeza kuwa anakusudia la kuhakikisha ndani ya muda mfupi Mkoa wa Dar es Salaam na maeneo mengine nchini yanatapakaa Bendera za CUF.
Kwa upande wake aliyekuwa Mwenyekiti wa ACT-Wazalendo Mkoa wa Dar es Salaam, Bw. Salum Rajab Sudi akizungumza kwa niaba ya wanachama waliorejea CUF kwa upande wa Tanzania Bara ameshukuru viongozi wa CUF kwa kuwapokea.
Amesema kuwa kupitia chama cha CUF wanaimani watapambania Watanzania kwamba wameamua kuja kukijenga chama na sio kutafuta vyeo.
"ACT-Wazalendo ndani ya miezi tisa watajua wapi panavuja, tutahakikisha Pemba tunairejesha ndani ya mikono salama ya CUF," alisema Bw. Sudi.



