Breaking News

TANGA BOYS MABIGWA MKUCHU CUP 2021/22.


Mgeni rasmi Meya wa manispaa ya Kinondoni mhe. Songoro Mnyonge akikabidhi nahodha wa timu ya Tanga Boys kombe la ushindi na Bodaboda kwa mshindi wa shindano la Mkuchu CUP 2021/22 yaliyofanyika katika  viwanja vya Machava, Kunduchi jijini Dar es salaam.
Mgeni rasmi meya wa manispaa ya Kinondoni mhe. Songoro Mnyonge akizungumza katika fainali ya Mkuchu CUP 2021/22 uliyofanyika katika viwanja vya Machava, Kunduchi jijini Dar es salaam
Mwandaaji wa mashindano Mkuchu CUP 2021/22 ambaye pia ni Mwenyekiti wa serikali ya mtaa wa Kilongawima, Bw. Emmanuel Mkuchu akizungumza mara baada ya katika fainali ya Mkuchu CUP 2021/22 Katika viwanja vya Machava, Kunduchi jijini Dar es salaam 
Mwenyekiti wa Taasisi ya bega kwa bega na mama bw. Mohamed Hassan kiongelea ushiriki wao katika mashindano MKUCHU CUP 2021/22 mashindano yaliyofanyika katika uwanja wa Machava Kunduchi jijini Dae es salaam
Mkuu wa kitengo cha masoko Meridian Bet bw. Twaha Ibrahim akifafanua jambo kwa waandishi wa habari mara baada ya kumalizika fainali MKUCHU CUP 2021/22 mashindano yaliyofanyika katika uwanja wa Machava Kunduchi jijini Dae es salaam.
Mkaazi wa kata ya Kunduchi Bi Twilomba-Jane Balama akiongea na waandishi wa habari baada ya kumalizika fainali MKUCHU CUP 2021/22 iliyofanyika katika uwanja wa Machava Kunduchi jijini Dae es salaam.
Timu za Tanga BOYS na Nondo FC zikiwa uwanjani.

Dar es salaam.
Fainali ya Michuano  ya mpira wa miguu ya MKUCHU CUP 2021/22 imemalizika rasmi huku timu ya Tanga Boys ya Kunduchi ikiibuka mshindi wa michuano hiyo kwa kuichapa timu ya Nondo FC yenye maskani yake Msisiri, Mwananyamala kwa goli 1 kwa 0.

Akizungumza mara baada ya kumalizika kwa mtanange huo meya wa manispaa ya Kinondoni, mhw. Songoro Mnyonge amewapongeza waandaaji wa michuano hiyo kwani imewaunganisha vijana si tu wa kata ya kunduchi bali wilaya nzima ya Kinondoni na Mkoa wa Dar es salaam kwa ujumla.

Mhe. Songoro amesema michuano kupitia michuano hii ya Mkuchu Cup imeonyesha ni jinsi gani vijana wanaweza kuungana kwa pamoja katika sekta ya michezo na kuunga mkono jitihada za Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan katika kuiboresha sekta ya michezo hapa nchini.

''Napenda kuwapongeza sana waandaaji wa michuano ya Mkuchu Cup 2021/22 kupitia ndugu yangu Emmanuel Mkuchu ambayo imeshatazamwa na karibia watu elfu 20 tangu Kuanza kwake,na niipongeze pia kampuni ya Meridian Bet na Taasisi ya bega kwa bega na mama hili nataka liwe mfano kwa kata na mitaa mingine kuandaa michuano ya namna hii ambayo huleta chachu ya michezo na ari kwa vijana'' Alisema Mhe Songoro.

Kwa upande wake mwandaaji wa michuano hiyo ambaye pia ni mwenyekiti wa serikali ya mtaaa wa Kilongawima, bw. Emmanuel Mkuchu amesema lengo la kuandaa michuano hiyo si tu kuwanganisha vijana kupitia michezo pekee bali kuwahamasisha wananachi kushiriki kikamilifu katika sensa ya watu na makazi inayotarajiwa kufanyika mwezi Agosti mwaka huu.

'Nikiwa kama kijana na kiongozi wa serikali za mitaa nilihamasika na nikaona si vibaya kuanzisha michuano hii kwa kushirikiana na Meridian Bet na Taasisi ya Bega kwa bega na mama kwa lengo la kuwahamasisha vijana na wanannchi kushiriki kikamilifu katika zoezi la sensa ya watu na makazi 2022 kundeleza juhudi za serikali katika kuletea Taifa letu Maendeleo'' Alisema Mkuchu.

Alisema michuano hii imehusisha timu 20 za ndani na nje ya Kunduchi ambapo mshindi wa kwanza  ambaye ni timu ya Tanga Boys imejishindia pikipiki yenye thamani ya zaidi ya milioni 2.6 na kombe la ushindi huku mshindi wa pili ambaye ni timu ya Nondo FC ikijinyakulia kitita cha shilingi milioni moja Taslim.

Naye Mwenyekiti wa Taasisi ya bega kwa bega na mama bw. Mohamed Hassan amesema taasisi hiyo imeamua kushirikiana na waandaaji wa Mkuchu Cup 2021/22 kumuungana mkono Rais Samia kuinua sekta ya Michezo nchini hivyo wao kama taasisi wataendelea kuwaunga mkono watanzania wote wenye mapenzi mema na Taifa.

Kwa upande wake mwakilishi wa Meridian Bet ambao ni moja ya wadhamini mashindano hayo, mkuu wa kitengo cha masoko bw. Twaha Ibrahim alisema michezo imekuwa chachu ya maendeleo kwa vijana ndiyo maana kampuni hiyo ikaamua kuidhamini mashindano haya ya Mkuchu Cup 2021.

Nae mkaazi wa kata ya Kunduchi Bi Twilomba-Jane Balama mmoja ya walioshuhudia fainali hiyo amemwomba Rais Samia kuendelea kuishika mkono sekta ya michezo sambamba na kumpongeza mwenyekiti wa serikali ya mtaa wa Kilongawima kwa uthubutu wake kupitia fainali hizo.