CLUB YA TP MAZEMBE YATAKIWA KUREJESHA MEDARI, KOMBE NA PESA WALIZOPEWA KAMA BINGWA 2021
Shirikisho la soka nchini Congo DRC FECOFA limeiamuru klabu ya TP Mazembe kurejesha medali,kikombe pamoja na pesa ambazo walipewa juni 2021 kama zawadi baada ya kutwaa ubingwa wa ligi kuu nchini humo na kuwapatia Klabu ya As Vita mara moja.
Fecofa wametoa siku 15 pekee kwa mabingwa hao ambapo wanatakiwa mpaka ifikapo machi 14,2022 wanatakiwa wawe tayari wamekabidhi vitu hivyo tajwa zikiwemp fedha ambazo ni dola za kimarekani laki moja ambazo walipewa na mdhamini mkuu wa ligi kampuni ya Vodacom.
TP Mazembe wamethibitisha kupata taarifa hiyo kutoka kwenye mamlaka ya soka nchini humo.
Mazembe wamepata kadhia hiyo kufuatia sakata lao la kumtumia mchezaji kinyume na taratibu jambo ambalo limewafanya Fecofa kuwavua ubingwa wa ligi kuu msimu 2020/21 TP mazembe.



