Breaking News

DKT. GWAJIMA AIPONGEZA SAUTI YA JAMII KIPUNGUNI KUPAMBANA NA UKATILI KIJINSIA

WAZIRI wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Dkt. Dorothy Gwajima akizungumza na wananchj pamoja na wadau wengine baada ya kumaliza ziara ya iliyoifanya mapa leo Machi 1, 2022 jijini Da es salaam.

Mwenyekiti wa Taasisi ya Sauti ya Jamii Kipunguni Bi. Fatma Talib akimkaribisha ofisini WAZIRI wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Dkt. Dorothy Gwajima ameipongeza taasisi leo Machi 1, 2022 jijini Da es salaam.
Mkurugenzi wa Taasisi ya Sauti ya Jamii Kipunguni Bw. Selemani Bishagazi akifafanuzi namna taasisi yake inavyofanyakazi na jamii kwa Waziri wa Jaamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maluum, Dkt. Dorothy Gwajima alipofanya ziara leo Machi 1, 2022 jijini Dar es salaam.

Dar es salaam.
WAZIRI wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Dkt. Dorothy Gwajima ameipongeza taasisi ya Sauti ya Jamii Kipunguni kwa kazi kubwa inayofanya ya kupinga ukatili katika jamii.

Dkt. Gwajima ametoa pongezi hizo leo Machi 1, 2022 alipotembelea na kujionea shughuli zinazofanywa na taasisi hiyo iliyopo Mtaa Amani Kata ya Kipunguni jijini Dar es Salaam kuelekea siku ya wanawake duniani ambayo hufanyika Machi 8 kila mwaka.

“Naipongeza taasisi ya Sauti ya Jamii Kipunguni kwa kazi nzuri inayoifanya ya kupambana na ukatili katika jamii yetu. Kwa kweli hili linafaa kuigwa na wadau wengine,” amesema Waziri Dkt. Gwajima.
Hata hivyo Wazir Dkt. Gwajima amesema kuwa tatizo la ukatili katika jamii halitaisha kwa kuzungumza na wanawake pekee juu ya tatizo hizo hilo bali kwa kuhusisha wanaume kwa nguvu zote.

“Tatizo la ukatili katika jamii, halitakwisha kwa kusema na wanawake pekee, bali hadi wanaume watakapotoka na kusema ukweli ili kuokoa mabinti zetu,” amesema Waziri Dkt. Gwajima.
Waziri Gwajima amewataka watu wenye matatizo kwenda kwenye taasisi hiyo kujifunza kazi wanayoifanya kwani ni mkombozi wa jamii katika kupambana na ukatili.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Taasisi ya Sauti ya Jamii Kipunguni Selemani Bishangazi amesema hadi sasa wameshafanya ufuatiliaji wa kesi mbalimbali za ukatili wa kijinsia.

Akizifafanua amesema “unyanyasaji ni 20, matunzo ya mtoto 20, mirathi 16, ukatili 19, madai 27, ukeketaji 3, ardhi 8, ubakaji 2, rushwa yangono 2, kutoa elimu 6, ndoa 17, jinai 3 na vitisho 2 na utapeli 1,”.
Akizungumzia kuhusu mapambano dhidi ya ukeketaji ameeleza kuwa mwaka 2014 waliokoa mabinti 19, mwaka 2016 mabinti 46, mwaka 2018 mabinti 34 na mwaka 2020 mabinti 16 ambapo jumla ni mabinti 115.

Aidha amebainishwa kwamba wamefanya mafunzo ya ujasiriamali ambapo wamefikia jumla ya watu 5650 ambapo wanawake ni 1600, wanaume 280 huku wenye mahitaji maalum wakiwa ni 120 na kubainishwa kwamba wanawake ni 82 wakati wanaume ni 38.