MALAGASHIMBA AMPONGEZA RAIS SAMIA KUANZISHA WIZARA YA MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WANAWAKE NA MAKUNDI MAALUM
Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Amani Kata ya Kipunguni wilayani Ilala jijini Dar es Salaam Daniel Malagashimba akifafanua jambo kwa wandishi wa mtandao huu mara baada ya Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum baada ya kutembelea kituo cha Sauti ya Jamii Kipunguni.
Dar es salaam:
MWENYEKITI wa Serikali ya Mtaa wa Amani Kata ya Kipunguni wilayani Ilala jijini Dar es Salaam Daniel Malagashimba amemshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuanzisha Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum.
Malagashimba ametoa pongezi hizo leo Machi 1, 2022 katika mahojiano na mwandishi wa mtandao huu mara baada baada ya ziara ya waziri wa Wizara hiyo Dkt. Gwajima kutembelea Taasisi ya Sauti ya Jamii Kipunguni iliyopo Katika Kata ya Kipunguni wilayani Ilala jijini Dar es Salaam.
Alisema Wizara hiyo ina jukumu kubwa la kuatetea haki za watoto na akina mama wanaokumbana na vitendo vya ukatili wa kijinsia.
“Mimi ni Mwnyekiti wa Serikali ya Mtaa Amania ambapo Mh. Waziri wa Maendeeo ya Janii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Dkt. Dorothy Gwajima amekuja kujionea mwenyewe jinsi tunavyofanya operesheni za kudhibiti ukatili wa kijinsia, Lakini pia nimshukuru sana Mh. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Mama yetu mpendwa Samia Suluhu Hassan kwa kuona umuhimu wa kuanzisha hii Wizara nyeti ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum kwa ajili ya kutetea haki za watoto na akina mama hususan kupinga ukatili,” Alisema bw. Malagashimba.
“Mimi kama mdau wa maendeleo na Mwenyekiti wa Mtaa ni jukumu langu kubwa kuhakikisha kuwa kuna usalama wa watoto na akina mama kwa kuhakikisha hakuna ukatili wa kijinsia mtaani kwangu,” ameongeza.
Ameeleza kuwa wakati akiwa nje nchi alitamani siku moja akirudi kutoka Marekani aweze kudhibiti na kuhakikisha kwamba ukatili wa kijinsia nchini Tanzania unapungua ikibidi kuutokomeza kabisa.
“Ndiyo maana nikaungana na Diwani mstaafu Mh. Msofe katika kuanzisha Kituo cha kutetea haki za watoto na akina mama kwa kupinga ukatili kijinsia kwa kushirikiana na mwanzilishi wa Kituo cha Sauti ya Jamii Kipunguni Ndugu Selemani Bishagazi,” amesema Malagashimba.
Amesema wameanza mwaka 2016 hadi leo hii wamefanikiwa kufikia hatua kubwa kwani wana matawi zaidi ya sita ambapo ameeleza kuwa matawi hayo yapo Kitunda, Msongola, Chanika, Pugu, Kivuled pamoja na Zingiziwa.
”Kote huko ni matunda ya Sauti ya Jamii Kipunguni, tumeeneza elimu ya kupinga ukatili, lakini mimi kwa vile ni Mwenyekiti wa Mtaa nimekuwa nikikamata watu wote wanaofanyia ukatili watoto na akina mama na kuwafikisha kwenye vyombo vya dola ili Sheria ichukue mkondo wake
Amesema ndio maana Waziri Dkt. Gwajima amevutiwa na jinsi wanavyofanya kazi na kuimarisha taasisi hiyo ya Sauti ya Jamii Kipunguni hadi ameamua kuitembelea ambapo amejionea mambo mengi yahusuyo harakati na ujasiliamali katika harakati za kupinga ukatili wa kijinsia.
Aidha amesema ameanzisha mkakati wa kuibua akina mama ambao wamekuwa wakichukua hatua ya kuhifadhi mabinti na wanawake ambao wamekuwa wakikumbana na ukatili.



