PROF. LIPUMBA: UCHAGUZI CUF KUANZA MEI 14
CHAMA cha Wananchi (CUF) kinataraji kuanza ramsi mchakato wa chaguzi wa ndani Mei 14 kuchagua viongozi wa ngazi mbalimbali.
Akisoma maadhimio ya kikao cha baraza la uongozi Mwenyekiti wa taifa wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba alisema Baraza Kuu la Uongozi la Taifa lilikutana katika kikao chake cha kawaida kati ya Machi 24 na 25 mwaka huu.
Alisema kaitka kikao hicho ajenda mbalimbali zilijadiliwa ikiwemo Chaguzi za Jumuiya zote za Chama kwamba Uchaguzi huo unatarajiwa kumalizika mwezi Oktoba 2023.
“katika kuhakikisha Wanachama wote wanaorejea nyumbani na Wanachama wapya wanashiriki kikamilifu katika ujenzi wa Chama, Baraza Kuu la Uongozi la Taifa limeyaweka kando masharti ya Ibara ya 116 kifungu kidogo cha 6 yaliyopo kwenye Katiba ya chama ya mwaka 1992 Toleo la 2019, na badala yake Baraza Kuu la Uongozi la Taifa limezingatia kifungu kidogo cha 7 kilichopo kwenye Ibara tajwa hapo juu,” alisema Prof. Lipumba
Hivyo amebainisha kwamba wanachama wapya ambao hawajatimiza muda wa miezi sita ndani ya Chama watapata fursa ya kugombea au kuteuliwa kuwa viongozi katika ngazi mbali mbali za Chama ilimuradi wawe wametimiza sifa nyingine za kugombea au kuteuliwa.
Kwamba kwa mujibu wa Katiba ya Chama Uchaguzi huu utafanyika kuanzia ngazi ya tawi, Kata/Jimbo, Wilaya na Taifa.
Kuhusu mabadiliko katika uongozi Profesa Lipumba ameeleza kwamba Baraza kuu la Uongozi la Taifa limejaza baadhi ya nafasi zilizokuwa wazi za Wajumbe wa Baraza Kuu kutokana na sababu mbali mbali.
Amesema kwa upande wa Zanzibar Baraza Kuu limewateua Hamad Masoud Hamad na Kona Vuai Haji na kwa upande wa Bara limemteua Juma Shaaban Nkumbi kuwa Wajumbe wa Baraza Kuu na nafasi nyingine zilizo wazi zitajazwa katika kikao kijacho cha Baraza Kuu.
Ameendelea kueleza, Baraza kuu la Uongozi la Taifa baada ya mashauriano na kujadiliana kwa kina limefanya mabadiliko madogo kwenye nafasi ya Katibu Mkuu ambapo limemchagua Hamad Masoud Hamad kushika wadhifa huo akichukua nafasi iliyokuwa inashikiliwa na Haroub Mohamed Shamis.
“Baraza Kuu limemshukuru Haroub Mohamed Shamis kwa kazi kubwa aliyofanya kama Katibu Mkuu katika kipindi kigumu baada ya kifo cha aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chama, Hayati Khalifa Suleiman Khalifa, na kukiwezesha Chama kushiriki kikamilifu katika Uchaguzi Mkuu wa 2020,” amesema.

Aidha amesema kuwa Baraza Kuu la Uongozi la Taifa limewathibitisha Mkurugenzi na Naibu Mkurugenzi wa Mipango na Uchaguzi walioteuliwa na Mwenyekiti hivi karibuni na waliothibitishwa ni Mwadini Jecha ambaye anakuwa Mkurugenzi, na Yusuph Mbungiro ambaye anakuwa Naibu Mkurugenzi.
Kuhusu maadhimisho ya miaka 30 toka kuasisiwa kwa Chama hicho, Menyekiti huyo wa CUF amesema Baraza Kuu la Uongozi la taifa limeazimia kusheherekea miaka 30 ya kuasisiwa kwa Chama ifikapo Novemba 21 mwaka huu.

“Baraza Kuu la Uongozi la taifa limeipitisha siku ya tarehe 21 Novemba ya kila mwaka kuwa ni siku ya CUF (CUF Day), na kwamba siku hiyo itaadhimishwa kila mwaka ili iwe kumbukizi kwa kizazi kilichopo na vizazi vijavyo juu ya kudai Haki Sawa na Furaha kwa Wananchi Wote,” amebainisha Profesa Lipumba.
Akizungumzia kuhusu utungaji wa Kanuni za uendeshaji wa mikutano ya hadhara ya Vyama vya Siasa ameeleza kwamba Baraza Kuu la Uongozi la Taifa limetoa wito kwa Serikali kutozuia mikutano ya hadhara kinyume cha sheria na katiba.
Amesema Baraza kuu limesisitiza kwamba suala la Kanuni lisitumiwe kama kisingizio cha kuendelea kuzuia mikutano ya hadhara kinyume cha matakwa ya Katiba na Sheria.