Breaking News

TAMPRO YAZINDUA "TAMPRO AJIRA PORTAL" KUSAIDIA VIJANA KUPATA FUNGUA ZA AJIRA

 

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira Dkt. Selemani Jafo akifafanua jambo kwa waandishi wa habari mara baada ya kuzindua TAMPRO Ajira Portal itakayosaidia vijana kupata fursa za ajira jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Jumuia ya Wanataalama Vijana wa Kiislamu (TAMPRO) akielezea namna TAMPRO Ajira Portal itakayosaidia kuwaunganisha vijana na fursa za ajira jijini Dar es Salaam
Baadhi ya vijana walioshiriki kongamano hilo ambalo pia ulifanyika uzinduzi wa TAMPRO Ajira Portal jijini Dar es Salaam

Dar es Salaam
WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira Dkt. Selemani Jafo amezindua rasmi TAMPRO Ajira Portal itakayosaidia kuwaunganisha vijana na fursa za ajira.

Akizungumza katika ufunguzi wa kongamano la vijana lililoandaliwa na Jumuiya ya Wanataalama wa Kiislamu Vijana (TAMPRO), Waziri Jafo aliipongeza TAMPRO kwa ubunifu huo wenye lengo la kusaidia vijana kupata ajira kwa urahisi.

“Nawapongeza kwa kazi kubwa mnayofanya ya kuunganisha vijana. TAMPRO imekuwa ikiunganisha vijana na kuwapa elimu na hamasa. Jumuiko hili linamanufaa makubwa kwani linajua changamoto kubwa ya vijana. Taasisi hii imeona umuhimu wa kukutanisha vijana na kuwaonesha fursa,” Alisema Mhe Jafo.

Alisema kila mwaka vijana wengi uhitimu vyuo na kwamba kwa mujibu wa soko la ajira si vijana wote wanaopata ajira.

“Niwapongeze sana kwa ubunifu wenu wa kuanzisha programu hii ya TAMPRO Ajira Portal maalum kwa ajili ya fursa za ajira kutoka Sekta Binafsi,” 

Mhe. Jafo alielezea kuwa changamoto ya ajira si kwamba ipo tu Tanzania bali ni changamoto ambayo inakabili mataifa mengi duniani.

Niwatake vijana kuchangamkia fursa hiyo kwani itawarahisishia kupata ajira na kwamba watakapopata wawe mabalozi bora wa program hiyo kwa kuhakikisha nanafanya kazi kwa bidiaa na kuacha alama ambayo itawafanya wakumbukwe.

Pia mhe Jafo amewataka vijana kuhakikisha wanajiandaa hili kuwa mahiri waweze kuajirika kwa urahisi  na wanapokuwa ‘field’ kuhakikisha wanatumia fursa hiyo kuongeza ujuzi ili wanapokuja kwenye soko la ajira wasipate vikwazo.

“Vijana mnaomaliza vyuo mjiendae vizuri, mkienda ‘field’ mhakikishe mnajiandaa vizuri na kuwa mahiri katika kazi. Tunapozindua hii Ajira Portal, vijana tumieni kutafuta fursa hii kupata ajira,” amesema Dkt. Jafo.

Aidha waziri Jafo ameuagiza uongozi wa TAMPRO kuhakikisha unashawishi makampuni viongozi wa taasisi pamoja na wastaafu kuangalia fursa za ajira katika program hiyo, kwa ajili ya kutoa fursa za ‘field’ pamoja na kuajiri vijana.

Nae Mwenyekiti wa TAMPRO, Bw. Haji Mrisho ametumia ufunguzi huo kuzitaja changamoto mbalimbali zinazowakabili vijana kubwa ikiwa ni upatikanaji wa ajira na kutoajirika kwa vijana wengi.

Alisema wao kama Asasi ya Kiraia wanaunga mkono juhudi za Serikali katika kukabiliana na changamoto ya ajira nchini.

“TAMPRO ni Asasi ya Kiraia inayounga mkono juhudi za Serikali. Tunafahamu kwa sasa Serikali kuna juhudi inafanya kupunguza changamoto ya ajira na hivi karibuni imetangaza fursa za ajira. Jambo la kujiuliza ni wangapi watapata fursa na wakipata watazitumikiaje".

Bw. Mrisho aliongeza kuwa TAMPRO badala ya kuwalaumu vijana wamekuwa wakiwajengea uwezo wa kuajirika, lakini pia wanawapa uwezo wa kujiajiri.

“Hili ndilo lengo kubwa katika kuunga mkono Serikali, hivyo tunawajengea uwezo vijana, tunawawezesha kupata taarifa zitakazo waunganisha na waajiri pamoja na kuwaunganisha na fursa za ajira,” Alibainisha bw.Mrisho.