ACT WAZALENDO SERIKALI ZIBENI MIANYA YA KUTOROSHWAJI WA MADINI
Chama cha Act Wazalendo kimetoa wito kwa serikali kupitia wizara ya madini kuendelea kuzuia mianya ya utoroshwaji wa madini kwa kuchukua hatua kali dhidi ya wahusika wa vitendo hivyo.
Akizungumza Jijini Dar es Salaam mara baada kuwasilishwa ya bajeti ya Wizara ya Madini Bungeni Jijini Dodoma Msemaji wa kisekta wa chama hicho, Edgar Mkosamali amesema serikali inatakuwa kusimamia kikamilifu utekelezaji wa sheria ya madini na kanuni zake.
Alisema kutokana na kushindwa kwa serikali kutekeleza matakwa ya sheria ya madini inayoitaka serikali kumiliki asilimia 16 ya hisa katika makampuni madini kumechangia kwa asilimia kubwa upotevu wa mapato ya serikali kutokana sekta ya madini.
Pia ameitaka serikali kuanza kutenga fedha katika bajeti yake walau asilimia tano kwa ajili ya kuwawezesha wachimbaji wadogo Tanzania ambao huchangia asilimia 30 ya pato la taifa kupitia sekta ya madini.
“Asilimia 30 ya mapato ya sekta ya madini yanatokana na wachimbaji wadogo ila hadi sasa serikali bado haiwajali ili hali sera inasema serikali itawezesha ili kukua kwa kuwaelimisha na kuwapatia mtaji na vifaa hivyo ni vyema serikali ikaanzisha benki ya madini ili isimamie mikopo na wachimbaji wadogo wa madini kwani ni vigumu kwa benki za kawaida kutoa mikopo kwa wachimbaji wadogo” Alisema bw. Mkosamali.
Aidha bw. Mkosamali ameshauri serikali kuziwezesha taasisi zilizo chini ya Wizara ya Madini ili ziweze kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi zaidi kwa kuendana na ukuaji wa sekta hiyo kwa kuendana na kasi ya mabadiliko ya kiteknolojia inayotumika duniani




