Breaking News

ACT-WAZALENDO YASHAURI KUUNDWA TUME HURU KUCHUNGUZA MATUKIO YA MOTO

CHAMA cha ACT-Wazalendo kimetaka kuundwa kwa Tume Huru itakayo washirikisha pia  wafanyabiashara wadogo wenyewe kuchunguza vyanzo vya masoko kuungua sehemu mbalimbali nchini na hatua mahususi za kuchukua kudhibiti hali hiyo.

Akizungumza jijini Dar es Salaam na Waziri Mkuu Kivuli wa chama hicho Dorothy Semu akizungumza na waandishi wa habari kufuatia hotuba ya bajeti ya Ofisi ya Waziri Mkuu kuhusu mapitio ya kazi na mwelekeo wa Serikali na makadirio ya matumizi kwa mwaka wa Fedha wa 2022/223.

Alisema Ofisi ya Waziri Mkuu ndio kisheria ndio inasimamia kukabili majanga nchini katika siku za hivi karibuni tumeshuhudia matukio ya masoko kuungua na kamati za kuchunguza kuundwa kila mara bila ya taarifa zake kuwekwa wazi huku matukio zaidi yamekuwa yakiendelea. 

“Kumekuwepo na taarifa kuwa matukio ya kuungua kwa masoko yanachomwa makusudi hili operesheni ya kuwaondoa wafanyabiashara wadogo isikamilike, minong'ono hii inaweza kuondoka kama itaundwa kamati ya uchunguzi huru kuchunguza kwani matukio haya yamekuwa yakiharibu mali za wananchi,” Alisema Bi. Semu

“Pamoja na matukio yote hutuba ya Waziri mkuu bado haijaonyesha matumaini yeyote ya kuipa nguvu Idara ya Maafa ili kuweza kuzuia masoko kuungua na hata majanga mengine nchini,”

Akizungumzia suala la kupanda kwa gharama za maisha kufatia kupanda kwa bei za bidhaa muhimu alisema kumekuwepo na vilio kutoka kwa wananchi kufatia kuwepo na hali ngumu ya maisha kutokana na kupanda bei kwa bidhaa zote muhimu ikiwemo chakula, petroli na dizeli.

“Tumeona bidhaa za chakula Ngano, Mchele, Mafuta ya kula vimepanda kwa wastani wa asilimia 60 hadi asilimia 180 nchi nzima, Vile vile kwa pembejeo za kilimo na Mbolea, vifaa vya ujenzi mwenendo wa bei upo juu zaidi. Katika hotuba ya Waziri Mkuu Bungeni suala hili halijapewa uzito unaostahiki,” ameeleza Semu. 

Amesema Serikali ni lazima ifunge mkanda wa matumizi yake na itoe nafuu kwa wananchi kwa kupunguza kupunguza ushuru wa forodha kwa mafuta ya kula na sukari na kodi hususani katika mafuta ya dizeli kwa angalau shilingi 500 kwa kila lita ya Dizeli ili kuwahami wananchi.