RC MAKALA AFUNGUA WIKI YA MACHINGA COMPLEX, AUPONGEZA UONGOZI KWA UBUNIFU HUO
Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam, Amos MAKALLA ameupongeza uongozi wa soko la Machinga Complex kwa kuandaa wiki ya machinga ambayo pamoja na mambo mengine kutakuwa na maonyesho ya biashara.
Akizungimza katika ufunguzi wa wiki hiyo Rc Makala alisema amefurashiwa sana na ubunifu wa viongozi wa soko hilo wiki hiyo na kuwaambia serikali ya wamu ya sita chini ya Rais Samia itaendelea kuhakikisha inawawekea mazingira wezeshi na salama kuwawezesha kufanya shughuli zao.
"Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na rais Samia inatambua mchango wa machinga na itaendelea kushiriana nanyi kuhakikisha inawawekea mazingira rafiki ya kufanyia shughuli zenu" Alisema Rd Makala.
Alisema rais Samia anawasalimu sana na anatambua mchango wenu ndio maana pamoja kuwa na majukumu mengi siku ya leo lakini kwa kutambua mchango na umuhimu wenu nimeona nifike hapa kufungua mwenyewe na kuwapa salamu kutoka kwa rais Samia.
Aidha mhe. MAKALLA pia ametumia nafasi hiyo kuwataka wanaopotosha wananchi kuwa soko hilo halina wafanyabiashara waache tabia hiyo kwani soko hilo lina wafanyabiashara lukuki wakiwemo wale waliotoka soko la kariakoo.
Mhe. Makala ameahidi kuendelea kuwa balozi mzuri na ataangalia namna wiki ya machinga kuwa tukio endelevu pia kuwaaidi kuendelea kulitangaza soko hilo lenye kila aina ya biashara huku akiwahakikishia kuendelea kulilinda soko hilo




