Breaking News

NGOME YA VIJANA ACT WAZALENDO YATOA UFAFANUZI MCHAKATO WA TUME HURU NA KATIBA MPYA

Ngome ya Vijana wa chama cha ACT Wazalendo imetoa ufaanuzi kufatia kuwepo na upotoshwaji wa kauli ya chama hicho kuhusu mchakato wa Tume huru ya uchaguzi na katiba mpya ambao umekuwa ukivuma katika mitandao ya kijamii.

Akizungumza jijini Dar es salaam, Mwenyekiti wa Ngome ya Vijana wa chama hicho Bw. Felix Kamgisha  Alisema kumekuwepo na uposhwaji mkubwa juu ya kauli iliyotolewa na kiongozi wa chama chetu kuhusu kuanza kwa mchakato wa Tume huru ya uchaguzi baada ya katiba mpya hivyo kinachoendelea katika mitandao kuwa kauli hiyo inaonyesha kutokutambua umuhimu wa katiba mpya sio kweli.

"Kumekuwepo na uposhwaji hasa katika mitandao ya kijamii juu ya kauli ya chama kufatia kutaka uanze mchakato wa Tume huru ya uchaguzi na kufatiwa na ikifatiwa katiba mpya kuwa ni kauli binafsi ya kiongozi wa chama jamii itambue kauli hiyo ndio msimambo wa chama" Alisema bw.Kamgisha

Alisema ACT Wazalendo wanatambua umuhimu wa katiba mpya hili chama kilikaa na kutafakali kwa kina na kuona uwepo wa tume huru unasaidia kuweza upatikanaji wa katiba mpya.

Bw. Kamgisha Aliongeza kuwa kwa mazingira ya sasa ya bunge letu lilivyo kama tutaanza na mchakato wa katiba mpya autakuwa na tija kutokana na bunge kuwa na wawakilishi wengi wa chama kimoja hivyo tukipata tume huru ambayo itawezesha kupatikana wawakilishi sahihi itasaidia upatikanaji wa katiba mpya bora