Breaking News

WASANII SALOME BONFACE NA JONGO MLOKOLE WAJA NA ALBUMU YA NYIMBO ZA KUSIFU NA KUABUDI ZENYE MAADHI YA SEGELI NA HIPHOP

Timothy Marko
Mwimbaji wa nyimbo za Injili Bi.Salome  bonface maarufu kama "Mama salehe " wa kanisa la ufufuo na Uzima amewataka wakristo nchini kusikiliza ujumbe wa nyimbo unaoleta ukombozi wa nafsi zao na sio kuvutiwa na mahadhi ya nyimbo.

Akizungumza na waandishi wahabari katika kanisa hilo jijini Dar es salaam amesema kuna tofauti kati ya nyimbo za Singeli na Taarabu inayopigwa kanisani na ya kidunia  taarabu ya kanisani ina maneno ya Mungu tofauti na ya kidunia.

"Taarabu ninayoimba mimi ni maneno ya kutoka kwenye biblia". Alisema Salome Boniface.

Alisema tayali amekamilisha Albamu yenye nyimbo tano ikiwemo Tanzania mpya na nyingine ni wimbo wa Ndoto.

Aliongeza kufikiasha mafundisho ya Neno la Mungu hakuna mipaka hivyo kwa kutambua hilo album yake aliyo ianda yenye nyimbo zenye mahadhi ya Singeli na Tarabu lengo ni watu wamjue Mungu kwa njia ya uimbaji.

Naye Msanii wa nyimbo za injili kwa mahadhi ya Hip hop, Jango Mlokole amesema hapo awali alikuwa katika mziki wa kidunia akimtumikia shetani lakini ameamua kumfuata yesu kristo na kumtumikia yeye kwa uimbaji kwa mahadhi hayo.

Alisema lengo la uimbaji ni kumwimbia yesu kristo na sio kupata fedha au kufanya biashara.

"Sisi hatufanyi biashara lengo la nyombo xangu ni kufundisha neno la Mungu, kuelimisha pamoja na kusifu na kuabudu Mungu".Alisema Jango.

Kwa upande wake Mchungaji Msaidizi wa kanisa hilo ambaye pia ni mwangalizi wa kanisa hilo, Bw. BarakaTegu amesema kumwimbia Mungu ni sanaa inayofikisha ujumbe ili watu wamrudie Mungu.

"Cha msingi  ni Maneno ya Mungu na sio Mahadhi ya Wimbo hivyo kupitia nyimbo hizi natumaini zitaweza kufikisha ujumbe wa neno la Mungu hasa kwa vijana". Alisema Mchungaji Muangalizi Baraka Tegu.