Breaking News

WATETEZI WA HAKI ZA BINADAMU WAPIGIA CHEPUO HAKI ZA WANAWAKE,WATAKA HAKI ZAO KULINDWA.

Na Timothy Marko
Mkurugenzi wa Tasisi ya Watetezi wa Haki za Binadamu (THRDC), bw Onesmo Olengurumwa amesema kati ya changamoto wanazopitia watetezi wa Haki za Binadamu wanawake ni pamoja kudhauliwa, kupigwa pindi wanapokuwa katika majukumu yao.

Akizungumza katika ufunguzi wa mkutano wa pili wa mwaka na uzinduzi wa Ripoti ya Hali ya watetezi wanawake wa haki za binadamu jijini Dar es salaam,  amesema wanawake wengi watetezi wa haki za binadamu wamekuwa wakipitia changamoto mbalimbali kama wakipingwa na kutukanwa pindi wanapotekeleza majukumu yao.

"Wanawake watetezi wa haki za binadamu na wanaotetea haki zao katika jamii wamekuwa wakiitwa majina mabaya hii ni moja ya changamoto kubwa wanayokutana nayo wanawake hivyo jamii inao wajibu wa kuwalinda pasipokujali jinsi yake" Alisema Olengurumwa.

Olengurumwa alisema mkutano huo wadau na washiriki watajadiliana juu ya changamoto mbalimbali wanazokutana nazo ikewemo changamoto za ukatili kwa wanawake na kuzitafutia ufumbumbuzi.

Alisema mkutano huo pia utazindua mpango kazi wa watetezi wa Haki za Binadamu wanawake kwa mwaka 2022 -2026 ambao unalenga kuweka mazingira wezeshi na salama kwa watetezi wanawake wa haki za binadamu nchini.

"Mkutano huu pia utajadiliana namna kuweka mazingira wezeshi na salama  kwa watetezi wanawake wa haki za binadamu na kuhakikisha haki za wanawake na wasichana zinalindwa."

Mkutano huo wa siku moja umewakutanisha wadau kutoka taasisi za Umma, Asasi za kiraia ambao wanafanyakazi za watetezi wa Haki za Binadamu wanawake nchini umebeba kauli mbiu ya mazingira wezeshi na salama kuhakikisha wanawake na wasichana wanalindwa.