Breaking News

CHAMA CHA ADC CHAUNGA MKONO HATUA ANAZOCHUKA RAIS SAMIA TANGU KUINGIA MADARAKANI

Mwenyekiti Taifa wa Chama cha Alliance For Democratic Change (ADC), Mhe. Hamad Rashid Mohamed akifafanua jambo katika Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Chama hicho uliofanyika 23 Mei jijini Dar es Salaam.

Dae es Salaam:
CHAMA cha Alliance For Democratic Change (ADC) kimempongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa hatua muhimu alizochukua katika kipindi kifupi cha uongozi wake.

Aizungumza katika mkutano mkuu wa mwaka Mwenyekiti Taifa wa Chama hicho, Mhe. Hamad Rashid amesema wajumbe wa kikao kwa kauli moja wanaunga mkono hatua zinazochukuliwa na sekali ya awam ya sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan katika nyanja za kisiasa na kijamii.

Amezitaja baadhi ya hatua hizo kuwa ni pamoja na kufungua milango yote ya kuviwezesha vyama vya siasa kufanya shughuli zake bila ya bugudha, vitisho au kubandikizwa mashtaka.

Nyingine ni kujiteremsha chini na kutembea katika kiapo na kauli zake kwamba ameunda Serikali kwa kuangalia uwezo, uzalendo na mahitaji bila kuangalia mhusika anatoka katika Chama gani au Taasisi gani.

“Hayo ameyafanya kwa vitendo, kwa kuweza kukutana na Viongozi wa vyama vya siasa katika vikao mbalimbali na hata kwa walioko nje ya nchi kwa lengo la kuendelea kujenga utaifa Wetu, ulio asisiwa na waasisi Wetu,” amesema Rashid na kuongeza kwamba,

“ADC mbali na kumpongeza kwa haya na mengine Mengi tunakuahidi kuendelea kukuunga mkono kwa vitendo kama ilivyo kawaida yetu katika mambo yote ya msingi wa kuendeleza Demokrasia ya kweli katika nchi yetu,”.

Amesema Chama hicho kimepokea kwa shauku kubwa dhamira yake ya kuanzisha Kikosi Kazi kitakacho mshauri juu ya mustakabali wa kuendeleza Demokrasia na Ustawi wa Siasa nchini.

Katika hatua nyingine amewataka wajumbe wa Mikutano Mkuu wa Chama kutambua kwamba jukumu lao la kwanza ni kujipanga vizuri katika kutimiza malengo ya Chama ambayo ni kushika dola.

“Hivyo naomba kuipongeza Ofisi ya Katibu Mkuu kwa kuandaa agenda ya mpango Kazi ambao utakiwezesha Chama chetu kufikia malengo yake kama kila mmoja Wetu atatimiza wajibu wake,” amesema Rashid.