Breaking News

NCCR-MAGEUZI NGOMA NZITO, WAPIGANA PINI

Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu Taifa ya Chama Chama cha NCCR-Mageuzi imekutana na kutoa maazimio manne ikiwamo kuwasimamisha nafasi za uongozi Makamu mwenyekiti Zanzibar, Ambar Hamid, mweka hazina, Suzan Masele na naibu Katibu Mkuu Zanzibar, Amer Mshindan.

Hatua hiyo imekuja siku moja  baada ya uliotambulishwa kuwa ni mkutano wa Halmashauri Kuu ya Chama cha NCCR-Mageuzi kutangaza kuwasimamisha Mwenyekiti wa Chama hicho, James Mbatia na makamu makamu mwenyekiti wake upande wa Bara,Angelina Mtahiwa.

Wajumbe wa kikao hicho wamekutana na kutoa maazimio manne ikiwamo kuwasimamisha nafasi za uongozi Makamu mwenyekiti Zanzibar Ambar Hamid, mweka hazina, Suzan Masele na naibu Katibu Mkuu Zanzibar, Amer Mshindan.

Akieleza juu ya maamuzi hayo ya Mwenyekiti wa Baraza la Wadhamini la Chama hicho, Mohamed Tibanyendela amesema wamewasimamisha Makamu mwenyekiti Zanzibar, mweka hazina, na naibu Katibu Mkuu Zanzibar hadi pale Halmashauri Kuu itakapokutana.

Pia amesema maazimio mengine ni kutotambua mkutano wa Halmashauri Kuu uliofanyika Mei 21, 2022 uliotoka na uamuzi wa kuwasimamisha viongozi wawili wa Chama, akidai kuwa ni kinyume na mujibu wa katiba.

 Ameongeza kuwa Chama hicho kuwa tayari kimemwandikia barua Msajili wa Vyama vya Siasa juu ya kusogezwa mbele kwa mkutano huo hadi mwezi Agosti 2022.

Itakumbukwa awali siku moja kabla ya kikao hicho cha Halmashauri Kuu kilichokutana katika ukumbi wa Jeshi la Wokovu uliopo Kurasini Jiji Dar es Salaam kilitangaza kumsimamisha Mbatia na Makamu wake upande wa Bara na kusema kuwa hawatakiwi kujihusisha na shughuli yoyote ya Chama.

Source Watetezi tv