Breaking News

KUFATIA KUTOWEKA ASKOFU MKUU KANISA LA HOUSE OF PRAYER SHIELD OF FAITH WAOMBA MSAADA WA SERIKALI KUJUA ALIPO

Kuhani wa Kristo wa Kanisa la House of Prayers Shield of Faith Christian Fellowship akifafanua jbo kwa waandishi wa habari Jijini Dar es Salaam kufatia jitihada za kumtafuta Askofu mkuu wa Kanisa hilo tangu kuchukuliwa kanisani hapo kisha kutoweka.
Mama Mteule wa Kanisa la House of Prayers Shield of Faith Christian Fellowship, Greener Mkombo  akifafanua jambo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) uliofanyika kanisani Boko Jijini Dar es Salaam.
Pichani ni Askofu mkuu wa Kanisa la House of Prayers Shield of Faith Christian Fellowship, Mulilege Kameka Maarufu (Mzee wa Yesu) ambayo anadaiwa ametoweka.

Dar es Salaam:
Kanisa la House of Prayers Shield of Faith Christian Fellowship limeiomba Serikali kusaidia kujulikana wapi alipo Askofu mkuu wa Kanisa hilo Mulilege Kameka maarufu kama Mzee wa Yesu.

Akizungumza jijini Dar es Salaam na Kuhani wa Kristo kwa niaba ya makuhani wote wa kanisa hilo nchi nzima, Nazar Nicholas amesema mpaka sasa ni Siku saba zimepita tangu kutoweka kwake.

“Tunaiomba Serikali kupitia idara zake na taasisi zake zitueleze na kutusaidia kujua Askofu Mulilege yupo wapi ili aweze kuhudumiwa kwani hadi sasa tumeshazunguka kila mahali ikiwemo kwenye vituo vya Polisi lakini hatujamuona,” Aliema Nicholas.

Alisema kufatia sintofahamu na baada ya jitihada zote za kumtafuta kutokuzaa matunda tumemua kuongea na vyombo vya habari Rais asikie pamoja na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi kwani tunaimani na mheshimiwa Rais ameshaiweka nchi kwenye Sheria.

Nicholas alisema kwa mara ya kwanza Jumatano iliyopita ndio walizingumzia kuwepo na sintofahamu hii kupitia vyombo vya habari bado hakuna jipya hadi leo juu ya taarifa za aliko Mzee wa Yesu.

“Tunaamini Serikali ina mkono mrefu hakuna kitu kinaweza kufanyika wahusika wasijue,” Alisema Nicholas.

Aidha Nicholas aliongeza kuwa wao wataendelea kumtafuta na kufanya maombi bila kuchoka ili kuhakikisha Askofu anapatikana.

Kwa upande wake Mama Mteule wa Kanisa hilo ambaye pia ni Mke wa Mzee wa Yesu, Greener Mkombo  amefichua kuwa tangu mwaka 2011 amekuwa askofu  akisumbuliwa kwa madai kwamba sio Raia wa Tanzania.

Asema tatizo hilo lilianza mara tu walipohamia jijini Dar es Salaam wakitokea mkoani Mbeya.

Hata hivyo amesema pamoja na hayo Mzee wa Yesu amekwisha shinda kesi na Mahakama Kuu kuthibitisha kwamba ni Mtanzania.

Hivyo amesisitiza Serikali kusaidia kupatikana kwa Mzee wa Yesu ili kama anashikiliwa kwa makosa yoyote aweze kufikishwa Mahakamani ili mkondo wa Sheria uchukuliwe.