Breaking News

MAPYA YAIBUKA GOGORO WA CHAMA CHA NCCR-MAGEUZI

Katibu Mkuu wa Chama cha NCCR-Mageuzi Bi. Martha Chiomba amesema kwa mujibu wa katiba ya chama yeye bado ni Katibu Mkuu wa Chama hicho na kuhusu swala la kujiuzulu alilazimishwa kufanya hivyo na viongozi wakuu wa chama.

Akizungumzia Jijini Dar es Salaam juu ya madhila aliyopitia baada ya kukataa kujiuzulu Katibu Chiomba amesema kulibuka mgogoro baina yake na baadhi ya viongozi wa chama hicho hususan Mwenyekiti James Mbatia ambao mpaka saivi unaendelea.

“Mimi bado ni Katibu Mkuu wa Chama cha NCCR Mageuzi na kwa sasa Chama kiko mikononi mwangu, tumeshindwa kuingia ofisini kutokana na uhuni wao bado hatua tunaendelea kuzichukua ili tuingie ofisini, nitaandika barua wanipe funguo, ikishindikana tutatumia utaratibu wa kisheria,” Alisema Chiomba.

Alisema kufatia Mhe. Mbatia na wenzake kusimamishwa na kitakiwa kutojihusisha na shughuli zozote za chama na asubiri kwenda kujitetea kwenye Mkutano Mkuu.

Akielezea mgogoro huo ambao ulianza Februari 17 mwaka huu pale alipoitwa nyumbani kwa Mwenyekiti huyo wa NCCR-Mageuzi na kutakiwa kujiuzulu nafasi yake ya Ukatibu Mkuu akielezwa kwamba kuna vijana ambao wanashinikiza jambo hilo.

Alisema aliambiwa kuwa vijana hao wanataka ajiuzulu kwa sababu ameshindwa kutekeleza majukumu yake hivyo anatakiwa kuchukua uamuzi huo ili kulinda heshima yake.

“Mara baada ya kuambiwa hivyo na Mwenyekiti akiwa pamoja na watu wawili wa chama, nilijiuliza nimeshindwa kutekeleza majukumu gani. Hivyo sikutaka kujiuzulu pale, niliwauliza nikaandike barua au niitishe vyombo vya habari ila walinijibu niandike barua lakini sababu nilikuwa mgonjwa niliwaambia nitaandika baada ya kupata nafuu ila Mwenyekiti alisema ataandika halafu ataniletea mimi kwa ajili ya kusaini tu,” amesema Chiomba.

Alisema kutokana na mazingira aliyokuwa akikabiliana nayo tangu Februari 17 mwaka huu aliamua kubadili namba ya simu kwa kuhofia usalama wake.

Bi Chiomba ameeleza kwamba kabla ya kujiuzulu kama alivyotakiwa, aliamua kuomba ushauri kwanza kwa baadhi ya viongozi wa chama hicho akiwemo Anthony Komu, ambapo alimshauriwa asifanye hivyo, jambo ambalo amedai lilimkasirisha Mbatia na kuambiwa kwamba ni msaliti kwa sababu amemueleza jambo hilo Komu.

“Mwenyekiti hakufurahia kitendo changu cha kumweleza sula hili Komu. Baadaye nilishughulikiwa na vijana kwa kutukanwa matusi ya nguoni na kuvuliwa nguo na viongozi akiwemo Mwenyekiti hawakukemea jambo hilo,” amesema Chiomba.

Aidha bi. Chiomba ameeleza kuwa kutokana na hali inayoendelea tangu kutakiwa kujiuzulu maisha yake yapo hatarini na kwamba kwa sasa hana mahali maalum pakuishi kutokana na hofu na tayari ameshatoa taarifa polisi mda wowote masuala ya kusheria yakikamilika atakwenda kufungua mashtaka hivyo taasisi za kutetea wanawake zimuunge mkono.

Ikumbukwe kuwa wakati Chiomba akisisitiza kwamba yeye ndiye Katibu Mkuu wa NCCR-Mageuzi ikumbukwe kwamba Mwenyekiti wa chama hicho anayedaiwa kusimamishwa James Mbatia hivi karibuni alieleza kwamba Chiomba alikwisha simamishwa na chama