Breaking News

ACT WAZALENDO YACHAMBUA MAPENDEKEZO TISA YALIYO WASILISHWA KATIKA KIKOSI KAZI CHA RAIS

Makamu Mwenyekiti wa chama cha  ACT Wazalendo, Bi. Dorothy Semo (katikakti) Katibu Ado Shaibu (Kushoto) na Mjumbe wa chama cha ACT Wazalendo Ismaeli Jusa katika picha ya pamoja
Makamu Mwenyekiti wa chama hicho Dorothy Semo akielezea baadhi ya mapendekezo ya chama hicho katika mkutano na waandishi wa habari juu ya uchambuzi na mapendekezo yaliowasilishwa na chama hicho katika kikosi kazi kulichoundwa na mhe Rais Samia kuhusu Demokrasia kwa kutoa marekebisho na mapendekezo katika vifungu mbalimbali vya sheria.
Katibu wa Chama cha ACT Wazalendo, Ado Shaibu akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari juu ya uchambuzi na mapendekezo yaliowasilishwa na chama hicho katika kikosi kazi kulichoundwa na mhe Rais Samia kuhusu Demokrasia kwa kutoa marekebisho na mapendekezo katika vifungu mbalimbali vya sheria.
Mjumbe wa chama cha ACT Wazalendo Ismaeli Jusa akifafanua jambo katika mkutano na waandishi wa habari juu ya uchambuzi na mapendekezo yaliowasilishwa na chama hicho katika kikosi kazi kulichoundwa na mhe Rais Samia kuhusu Demokrasia kwa kutoa marekebisho na mapendekezo katika vifungu mbalimbali vya sheria.

Da es salaam:
Chama cha ACT Wazalendo kimechambua mapendekezo 9 ya kikosi kazi cha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuhusu Demokrasia kwa kutoa marekebisho na mapendekezo katika vifungu mbalimbali vya sheria.

Akizungumza na waandishi wa Habari leo Jijini Dar es Salaam Makamu Mwenyekiti wa chama hicho Dorothy Semo amesema vyama vya siasa vinapaswa kupewe jukumu la kutoa elimu ya uraia kwa wananchi.

Aidha amesema suala la uwepo wa wanawake katika ngazi za uongozi wa juu linapaswa kuzingatiwa na vyama vya siasa pamoja kuwekwa sheria ambayo inawataka kutimiza wajibu huo.

Ameongeza kuwa suala la rushwa liendelee kusimamiwa na mamlaka ya kuzuia na kupambana na rushwa TAKUKURU kabla na baada ya uchaguzi.

Kwa upande wake Mjumbe wa chama hicho Ismaeli Jusa amesema suala la katiba mpya sio swala la mjadala tena ndani ya chama hivyo hoja ya Katiba mpya haikwepeki kinachotakiwa ni maoni ya wananchi ambayo yanakidhi mahitaji ya mfumo wa Demokrasia ya vyama vingi.

Aidha amesema tayari kazi hiyo ilishaanza na mchakato huo ulikwamishwa baada ya kujikita kwenye masuala ya kisiasa ambapo chama cha CCM kupenyezwa vipande vipande katika bunge Maalumu la katiba zaidi kuliko kubeba maoni ya Wananchi hivyo kukosa sifa ya kubeba muafaka wa Taifa.

“ACT inahitaji katiba mpya na mchakato uanze sasa sambamba na hatua za kufanya mabadiliko ya msingi yatakayokidhi mahitaji ya muda mfupi na wa kati kuelekea uchaguzi wa serikali za mitaa na vijiji kupitia rasimu ya katiba mpya inayotokana na maoni ya wananchi kama yalivyotafsiriwa na kuratibiwa na Tume ya mabadiliko ya katiba ikiongozwa na Jaji Joseph Warioba “Alisema Jusa.

Ameongeza kuwa Makundi mbalimbali ya watu yashirikishwe hususani katika maeneo yanayobishaniwa ikiwemo suala la Muungano pamoja ba madaraka ya Rais.

Amesema Sheria ya uchaguzi inapaswa kufanyiwa marekebisho kwa kutowaruhusu wakurugenzi kuhusika kusimamia uchaguzi na Tume ipewe mamlaka ya kuajiri watu na isimamie uchaguzi wa serikali za mitaa badala ya kusimamia na TAMISEMI.

Aidha mapendekezo hayo yamependekeza kufutwa kwa Kifungu cha kura ya mapema Zanzibar ili kuondoa kutokuaminiana na mawakala kuruhusiwa kutumia simu wakati wa upigaji kura na uapishwaji wa mawakala ufanyike siku 3 kabla ya wameshaapishwa na vifaa vyote vya uchaguzi viwepo kabla siku ya uchaguzi.

Hata hivyo amesema Chama cha ACT Wazalendo kimependekeza kuwa ili kujenga Maridhiano kuwe na jukwaa la mazungumzo kupitia kituo cha Demokrasia Tanzania TCD na kipewe nguvu kisheria ya kutekeleza hilo tofauti na ilivyo sasa.

Naye Katibu Ado Shaibu amesema katika sheria ya vyama vya siasa kuhusu mikutano ya hadhara sheria inavipa vyama kufanya mikutano na Jeshi la polisi kazi yake ni kupewa taarifa tu na liwekewe mashariti ya mda wa kujibu na vikao vya ndani visihusishwe na jeshi la polisi.

Aidha amesema Ruzuku kwa sasa ni kwa vyama vichache hivyo wanapendekeza kuongezwa kwa vyama vinavyopata Ruzuku kwa kuzingatia utendaji wa vyama hivyo ikiwemo kushiriki katika chaguzi na kushinda walau Diwani au Mbunge mmoja pamoja Sheria kutaji kiwango cha upatikanaji wa Ruzuku na chama kitakachopata ruzuku kisiwe na hati chafu na kama hakina asilimia 30 ya wanawake kwenye viongozi wake.