MBATIA NA WENZAKE MARUFUKU KUJISHUGHULISHA NA NCCR - MAGEUZI
OFISI ya Msajili wa Vyama vya Siasa nchini Tanzania, imemliga marufuku aliyekuwa Mwenyekiti wa Chama cha NCCR-Mageuzi, James Mbatia na wenzake wanaodaiwa kuvuliwa nyadhifa zao, kuendelea na shughuli za siasa za chama hicho kwa kuwa sio kiongozi.
Akizungumza mapema leo 25 Mei Jumatano, jijini Dar es Salaam na Naibu Msajili wa Vyama vya Siasa, Sisty Nyahoza, akitangaza msimamo wa ofisi yake kuhusu maamuzi ya kikao cha Halmashauri Kuu ya NCCR-Mageuzi, kilichofanyika Jumamosi iliyopita, ya kumsimamisha uenyekiti Mbatia na sekretarieti yake.
"Kwa mujibu wa kifungu cha 8B cha Sheria ya Vyama vya Siasa, ni kosa kwa mtu yeyote kufanya shughuli za siasa kwa jina la chama ambacho yeye siyo kiongozi. Kufanya kitendo hjcho ni kosa la jinai, hivyo ninawaasa Mbatia, Angelina John Mutahiwa, Anthony Komi na wanachama wengine wa NCCR-Mageuzi waliokiwa wajumbe wa Sekretarieti iliyovunjea tarehe 21 Mei 2022, kutojifanya ni viongozi kwani kufanya hivyo ni kosa la jinai," imesema taarifa ya Nyahoza.
Taarifa ya Nyahoza imesema, kikao kilichomsimamisha uongozi Mbatia na wenzake kilikuwa halali kwa kuwa akidi yake ya wajumbe ilitimia kwa mujibu wa sheria




