Breaking News

MTANGAZAJI WA ITV AIBUKA MSINDI WA JUMLA TUZO ZA EJAT 2021


Masekepa Natisa Asangama  wa  Kituo cha Runinga  cha  ITV ameibuka Mshindi wa Jumla wa Tuzo za Umahiri wa Uandishi Habari Tanzania (EJAT) kwa mwaka 2021.

Aliwashinda wanahabari wengine watatu  – Nusra Kichongapishi  wa runinga ya mtndaoni ya TIFU , Sanula Athanas  wa  Nipashe  Herieth Makweta  wa Mwananchi. 

Ansangama  alishinda tuzo mbili  - Tuzo ya Wazi na Utalii na Uhifadhi  kwa runinga.

Alitangazwa Mshindi wa Jumla wa EJAT na Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye katika kilele cha tuzo hizo kwenye Hoteli ya Serena Jijini Dar es Salaam Mei 28,2021. 
Waziri  alimkabidhi  Mshindi huyo wa Jumla Tuzo, cheti  na hundi ya mfano ya kiasi cha sh. Milioni 3.

Fedha hizo zimetolewa na mshiriki kiongozi wa EJAT , Baraza la Habari  Tanzania, kumwezesha  mshindi huyo kujiendeleza kwa masomo.
Kushinda Tuzo ya Wazi  aliwashinda watangazaji wawili wa kituo cha runinga cha Star – Naishook Alais Makaseni  na  Sudi Shaaban  Ally  na kwa Tuzo ya Uhifadhi na Uhifadhi alikuwa mteule pekee.

Nusra  alikuwa mteule pekee  na kushinda Tuzo ya  kilimo na Biashara ya Kilimo kwa  vyombo vya habari vya mtandaoni na piaalishinda Tuzo ya Elimu, ambapo Athanas alishinda Tuzo ya Sayansi na Tuzo ya Haki za Bindamu na Utawala Bora na Herieth  alishindaTuzo za Hedhi Salama na Afya. 

Kushinda  Tuzo ya Sayansi  na Teknolojia , Athanas  alimshinda To win  Elizabeth  Edward Kusekwa wa Mwananchi  wakati  Herieth  Makweta  alikua mteule pekee  kwa Tuzo ya Hedhi Salama na alimshinda  Khamisuu Abdallah Ali  wa  Zanzibar Leo  na Christina  Mwangakale  wa The Guardian.

Ephrahim Edward Bahemu wa  Mwananchi  alishinda Tuzo ya Uchumi, Biashara na Fedha  akimshinda  Francis Dhamira Kajubi wa The Guardian  na  Mariam Shaban Mbwana  wa Mwananchi.

Michezo na Utawala  Tuzo yake ilitwaliwa na Maryam Salum Habib  wa  Zanzibar Leo  akimshindwa mwandishi mwingine wa gazeti hilo  Hanifa Salim Mohamed.

Kwa Radio Tuzo hiyo imeenda kwa  Said Seleman Lufune  wa City FM  aakimshinda  Adam Gabriel Hhando wa CG FM wakati  Paschal Michael  Buyaga wa TBC1 tuzo hiyo kwa runinga akimbwaga   Amour Khamis Ali  wa Zanzibar Cable TV.

Aurea Simtowe  wa  Mwananchi alishinda Tuzo ya Elimu kwa magazeti akimshinda mwandishi mwenzake  wa Mwananchi  Tumaini Msowoya  na  Abdi Juma Seleman  wa Zanzibar Leo.

Naishhoki Alais Makasemi  wa kituo cha runinga cha Star alishinda Tuzo ya Elimu . 

Beatrice Philemon Mkocho  aloshinda Tuzo ya Utalii na Uhifadhi kwa magazeti  wakati Najjat Hajj Omar wa   The Chanzo – online alitwaa Tuzo hiyo kwa vyomvo vya habari vya mtandaoni.

Tuzo ya Uandishi wa Habari za Uchunguzi ilitwaliwa na  Salum Vuai Issa  wa Zanzibar Leo.

Uandishi wa Habari wa Data Tuzo  yake ilitwaliwa na Francis Dhamira Kajubi wa  The Guardian  akimshinda  Ephrahim Edward Bahemu wa Mwananchi.

Isakwisa Njole Mbyale wa Highlands FM Radio alitwaa Tuzo  hiyo kwa   Redio ambapo Khalifa Said Rashid wa  The Chanzo alishinda  tuzo kwa  vyomvo vya habari za mtandaoni akimshinda   Daniel Samson  wa   Nukta Habari Blog.

Joe Beda Rupia  wa Jamhuri alishinda Tuzo ya Utawala Bora na Uwajiobikaji kwa magazeti  ambapo  kwa runinga TRuzo hiy ilitwaliwa na   Sudi Shabaan Ally wa Star TV   na  Lukelo Francis Haule wa  The Chanzo alishinda tuzo  hiyo pia.  

Halfan Chusi  wa Nipashe   na mwandishi mwingine wa Gazeti hilo   Sanula Athanas waliwashunda  wateule  wengine wawili   -  mfa yakazi mwenzao    Marco Zephania Maduhu  na mwandishi mwingine Hadija Rajabu kushinda tuzo  ya Haki za Binadamu na Utawala Bora.  

Tuzo ya Mpiga Picha Bora  kwa Magazeti  ilitwaliwa na  Sabato Mwafiri Kasika wa Nipashe wakati  Munira Abdillah Hussein  wa BBC Swahili alishinda Tuzo ya Mpiga Picha  Bora Runinga   akiwashinda Festo Charles Lumwe  wa Dar 24  na  Peter Simon Rodgers wa ITV.
Muhidini Ally Msamba  wa  The Guardian  alishinda  Tuzo ya Mchora Katuni Bora kwa  Magazeti.

Amina Ahmed Mohamed wa Zanzibar Leo aliwashinda  wanahabari wawili wa Nipashe  - Mary Geofrey Mashina na Augusta Mathias Njoji kutwaa Tuzo ya Jinsia na Watoto. 
 
Kwa Redio Tuzo  hiyo iliendwa  kwa  Gladness Joseph Msetti wa U FM Radio ya Azam Media  akimshinda Adam Hhando wa CG FM.
Kwa vyombo vya mtandaoni  mshindi wa Tuzo ya  Jinsia na  Watoto ni Harith Jaha Ally . 

Tuzo ya  kuripoti Gesi, Mafuta na Uchimbaji Madini imetwaliwa na  Joyce David Joliga  wa The Citizen  akimshinda  Elizaberth Cornery Zaya  wa Nipashe. Kwa vyombo vya habari vya mtandaoni  Tuzo  imeenda kwa  Mariam Ngollo John  wa Nukta Habari Blog.

Irene Nicholaus Mwasomola  wa Uhuru  alishinda Tuzo ya Kuripoti Watu Wenye Ulemavu akiwashinda  wateule wengine wawili- Habiba Zarali Rukuni  na Haji Nassor Mohamed wa Zanzibar Leo.

Tuzo ya Afya  kwa Redio imetwaliwa na Adam Gabriel Hhando wa CG FM  akimshinda  Isakwisa Njole Mbyale  Highland FM  Radio.
Jackline  Inyas Silemu wa ITV  alishinda Tuzo  ya Afya na  mtandaoni Tuzo hiyo imeenda kwa  Zuhura Hassan Makuka wa Dar 24.

Tuzo ya Hedhi Salama kwa Redio imeenda kwa Peter Lugendo John  wa  TBC FM  akiwashinda  wateule wengine wawili Jecha Simai Jecha wa  ZBC FM na Lugendo Ibrahim Madege wa UFM Radio.

Kwa  runinga  tuzo  hiyo imeenda kwa  Salma Msichoke Mrisho wa  Star TV akimshinda mfanyakazi mwenzake Omary Hussein Omary.
Baraka Jailos Messa wa  Habari Leo  alishinda Tuzo ya Ushirika  ambapo  kwa Rdio Tuzo hiyo imetwaliwa na won the Reporting Martha Stephen Nalimi wa Shamba FM.

Elizabeth Edward Kusekwa  wa Mwananchi  alishinda Tuzo ya Kundi la Wazi kwa magazeti akimshinda  Marco Zephania Maduhu.

Haji Nassor Mohamed wa  Pemba Today  alishinda  Tuzo ya Kundi la Wazi kwa  vyombo vya mtandaoni.