Breaking News

TAASISI YA WANAWAKE LAKI 1 YAMPONGEZA RAIS SAMIA

Taasisi ya Wanawake 100,000 imempongeza Rais wa awamu ya Sita wa Jamhuri ya Muungano ea Tanzania mheshimiwa Samia Suluhu Hassan kwa kuongeza mishahara ya asilimia 23.3 iliyotangazwa siku chache zilizopita.

Akizungumza na waandishi wa habari katika hotel ya Hyatty Kempinsk jijini Dar es salaam, Mkurugenzi wa haki za wanawake Bi. Josephine Matiro amesema uamuzi wa Rais Samia kuongeza ya asilimia 23.3 kama ongezeko la mshahara ni jambo la kupongezwa na kubwa kuwahi kutokea nchini.

Amesema ongezeko hilo ni kikubwa ukilinganisha na nchi nyingine za ukanda wa afrika ya mashariki na amekuwa mfano kwa mataifa mengine kwani zaidi ya miaka 7 sasa watumishi hawakuwahi kuongezewa mishahara nchini.

“Ongezeko hili limekuja katika wakati muafaka kutokana na kupanda kwa gharama za maisha pia litaongeza hali ya utendaji wa kazi kwa watumishi na kuwapa motisha kubwa ya kuchapa kazi kwa bidii zaidi na yote haya yanafanyika ikiwa ni mwaka mmoja tu tangu Rais aingie madarakani tunampongeza sana sisi kama wanawake laki moja tumeona tusinyamaze”. Alisema Bi. Josephine

Bi. Josephine aliongeza kuwa rais Samia tangu aingie madarakani amekuwa hakichukua hatua mbalimbali kama vile kutoa ajira katika sekta za elimu na afya, kutatua tatizo la mafao kwa watumishi, kuongeza umri wa wategemezi katika bima ya afya toka miaka 18 hadi 21 pamoja na kuwapandisha cheo watumishi wanaostahili kupandishwa vyeo.

Kwa Upande wake Mkurugenzi wa Miradi wa Taasisi hiyo ambaye pia ni balozi wa Utalii, Bi. Nangasu Warema akiuzungumzia filamu ya Royal Tour amesema Rasi Samia amefanya jitihada kubwa sana katika kutangaza utalii na matunda yake yameanza kuonekana.

Alisema kupitia Royal Tour vivutio vya utalii hapa nchini vemetangazwa sana hasa mlima Kilimanjaro ambao upo hapa nchini ambapo swali kulikuwa na taarifa zenye nia ovu kuutangaza kuwa mlima huo upo Kenya hivyo kwa sasa wageni wengi wameanza kuonekana kuingia nchini siku chache baada ya uzinduzi wa filamu hiyo.

“Kiukweli Rais wetu amefanya kazi kubwa, sisi kama wanawake wa Tanzania  tumevutiwa sana na Royal Tour ambayo tayali imeanza kuleta manufaa kwa nchi yetu na hiyo yote ni jitihada za mwanamke hodari na shupavu na tunaimbia dunia kuwa Tanzania tuna Rais mwanamke na ambaye ametangaza vyema nchi yetu kimataifa kwani zaidi ya chanel za televisheni 350 na majukwaa makubwa ya kuonyeshea sinema imeonyesha filamu hiyo pia kupitia mtandao wa Amazon na haya ni matokeo mazuri”alisema Bi Warema.

Katika hatua nyingine Bi Warema aliongeza kuwa wanawake 100,000 wameandaa mpango kabambe wa kutembelea vivutio vyote vya utalii hapa nchini huku akiwataka wanawake kushirikiana nao katika kuzunguka katika vivutio vya utalii ili kuitangaza nchi.

Kwa upande wake mwenyekiti wa Taasisi ya wanawake 100,000 Bi. Vicky Kamata amesema wanawake tunapaswa kujivunia Rais Samia na wanapaswa kuondoa fikra kuwa wao ni watu tegemezi kwa kuamini kuwa wanaweza kufanya mambo makubwa na waitumie filamu ya Royal Tour na uchapa kazi wa Rais kama mfano na msingi wa kutokata Tamaa.