TALGWU YAMPONGEZA RAIS SAMIA KWA KUWAHAKIKISHIA NYONGEZA YA MISHAHARA
Katibu mkuu wa chama cha Wafanyakazi wa Serikali za Mitaa Tanzania (TALGWU) amepongeza kauli iliyotolewa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan katika maadhimisho ya siku ya wafanyakazi duniani (MEI MOSI) ya kuwahakikishia nyongeza ya Mishahara watumishi wa umma nchini.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam amesema chama kimefarijika na na kinaunga mkono kauli ya Rais kwani ameonyesha anayo dhamiria dhati kuimarisha maslahi ya watumishi.
“Chama kinaunga mkono kauli ya mhe. Rais kwa ahadi aliyotoa katika kilele cha Mei Mosi jijini Dodoma ambayo imeleta matumaini mapya kwa wafanyakazi ambayo yalikuwa yamepotea kwa miaka mingi sana,” Alisema bw.Mtima.
TALGWU tunayo imani kubwa na wafanyakazi wote kwa ujumla tumefarijika kuona Mkuu wa nchi anatambua na kuthamini kazi kubwa wanayofanya katika kuleta maendeleo ya taifa nichukue nafasi huu kumshukuru Rais Samia kwani hiki ni kilio cha mda mrefu kwa muda watumishi wa umma.
“Hiki kilikuwa ni kilio chetu cha muda mrefu ambapo sasa jambo hili linaenda kutekelezwa kama alivyosema Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan,” Alisema Mtima.
Katika hatua nyingine bw. Mtima amemshukuru Rais kwa kusikilizia kilio chao cha muda mrefu kuhusu watumishi walioondolewa kazini kwa vyeti vya kughushi (Feki).
Alisema chama kwa kupitia TUCTA kwa muda mrefu walikuwa wakiiomba Serikali kuliangalia kundi hilo la Watanzania ambao walitumikia kwa uadilifu nchi lakini kwa bahati mbaya wakakumbwa na kadhia hiyo.
“Tunamshukuru Rais kwa kuonesha Upendo mkubwa kwa Watanzania ambao waliitumikia nchi yetu kwa nguvu zao zote hatimaye ameagiza Wizara ya Fedha na Mipango kushughulikia na kuwalipa stahiki zao zinazotokana na makato ya Mishahara yao,” alisema Mtima.
Vile vile wamemshukuru Rais Samia kwa kuagiza mifuko ya hifadhi ya jamii na maafisa utumishi kuhakikisha wanashughulikia haki na stahiki za watumishi wanaotarajiwa kustaafu ndani ya miezi sita ili pindi inapofika mtumishi anastaafu mafao yake yawe tayari.
Kadhalika TALGWU imetoa shukrani za thati kwa Rais kwa kuundwa kwa bodi ya kima cha chini cha mishahara kwa Sekta ya umma ambayo amesema imeanza kufanya tathmini ya Mishahara iliyopo sasa na kuagiza Wizara zinazohusika kuiwezesha bodi hiyo ili kutekeleza majukumu yake ipasavyo.
Aidha amemshukuru Rais kwa kukemea kitendo cha baadhi ya Wafanyabiashara kutafuta visingizio vya kupandisha kiholela bei za bidhaa.




