Breaking News

WAZIRI GWAJIMA AITAKA JAMII KUTOA TAARIFA JUU YA VITENDO VYA UKATILI

Na Timothy Marko
Waziri wa Maendeleo ya jamii jinsia Wanawake na watoto Dkt. Dorothy Gwajima ameitaka jamii kutoa taarifa za vitendo vya ukatili kwa Kamati ya Ulinzi na usalama ili kukomesha vitendo vya ukatili.

Akizungumza na kongamano la kupinga vitendo vya ukatili jijini Dar es Salaam Dkt. Doroth Gwajima ameitaja mikoa ya Arusha Dodoma  pamoja na Iringa kuwa imekuwa ikiongoza kwa vitendo vya ukatili ambapo watoto 1875 idadi hiyo imepungua 1549 ambapo baadhi ya watoto hao ulala kwenye Vituo vya Mabasi.

"Watoto wengi ambao hufanyiwa ukatili nikutokana kukosa malezi ya wazazi, ambapo wengi husafiri kwa njia za hatarishi  kwenye Chase's za magari". Alisema Waziri Dk Dorothy Gwajima.

Gwajima Alisema ipo haja kwa jeshi la polisi kufanya oparesheni kwenye Magari hususani yanayotokea mikoani kwani watoto wamekiwa wakisafirishwa peke yao pasipo Uangalizi.

"Kamati za wilaya katika waunde Kamati ya kudhibiti watoto mitaani Kamati iwe na wajumbe 10 ili kuweza kuwa na mifumo Maaluum kudhiti vitendo vya ukatili wa mtoto". Aliongeza Dorothy Gwajima.

Katika hatua nyingine waziri Gwajima amesisitiza kuwachukuliwa hatua kwa walezi na wazazi wote watakaobainika kuwatelekeza watoto.

Naye Mkuu wa polisi wa kituo Cha polisi Chang'ombe, ACP Riziki Makwaya Hali ya ukatili kwa watoto huanzia kwenye Familia ambapo kumekuwa na udhaifu wa ufuatiliaji kwa watoto.

Alisema watoto wengi upita vitendo vya ukatili kutokana kuangalia Video za ngono Mitaani.

Kwa upande wake Mkuu wa wilaya wa Temeke Joket Mwegeleo amesema atakwenda kutekeleza agizo la Waziri huyo.