WAZIRI MKUU MAJALIWA MGENI RASMI MAADHIMISHO YA 7 YA WIKI YA UTAFITI NA UBUNIFU UDSM
Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam,Prof. William Anangiisye (katikati) akifafanua jambo kwa waandishi wakati akitoa taarifa kuhusu maadhimisho ya saba ya Wiki ya Utafiti na Ubunifu yatakayoanza Mei 24 hadi Mei 26,2022. (Picha na Yusuph Digossi)
Dar es salaam:
Waziri mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Kassim Majaliwa anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika maadhimisho ya saba ya wiki ya utafiti na ubunifu ya chuo Kikuu cha Dar es Salaam ambayo yatafanyika kuanzia tarehe 24 hadi 26 Mei katika eneo la Maktaba mpya kampasi ya Mwalimu Julius Nyerere
Akizungumza jijini Dar es salam Makamu Mkuu wa Chuo cha UDSM, Prof William Anangisye Amesema chuo kutatumia maadhimisho hayo kama fursa ya kujipambanua katika Utafiti ambao ni mojawapo ya majukumu yake makuu kwa kuonesha shughuli zake za Utafiti, Ubunifu, Huduma kwa jamii na ubadilishaji maarifa Kama njia ya kutatua changamoto mbalimbali zinazo kabili jamii nchini hasa katika malengo ya serikali.
"Nichukue nafasi hii kuwataarifu na kuwaalika wadau na watanzania wote kwa ujumla kushiriki katika Maadhimisho ya Saba ya wiki ya Utafiti na Ubunifu kuanzia tarehe 24 Hadi 26 Mei katika eneo la Maktaba Mpya, Kampasi ya Mwalimu Julius Nyerere." Amesema Prof William Anangisye
Alisema Kati ya Utafiti na Ubunifu zaidi ya 300, mwaka huu chuo kitaonyesha zaidi ya miradi 103 iliyofanya vyema zaidi Kama vile mradi wa maabara ya kidijitali.
"Maadhimisho haya yatatoa Fursa ya kuimarisha Ushirikiano baina ya chuo na wadau mbalimbali kitaifa na kimataifa na kwa kuzingatia Hilo, Siku ya pili ya Maadhimisho kutakuwa na Mjadala Maalumu wa Ushirikiano na kimkakati utakaoshirikisha wadau kutoka katika sekta binafsi na za Umma" Amesema Prof William.
Prof William aliongeza kuwa wiki hiyo ya Maadhimisho ya Utafiti na Ubunifu itatumika pia kutambua michango iliyotukuka ya wataaluma na wanafunzi wa Chuo kikuu Cha Dar es salaam katika Utafiti, Ubunifu na ubadilushaji wa maarifa.
Maadhimisho haya yatafugwa tarehe 26 Mei 2022 na Waziri wa Elimu, sayansi na Teknolojia Mhe, Profesa Adolf Faustine Mkenda atawatunuku tuzo watafiti na wabunifu Bora katika makundi tofauti tofauti.




