Breaking News

YUNA TANZANIA KUFANYA KONGAMANO KUBWA LA VIJANA


Mwenyekiti wa YUNA Tanzania, Hortancia Nuhu akongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) mara baada ya ufunguzi wa mkutano wa vijana  kujadili ushirikishwaji wa vijana kuhusu masuala ya afya ya uzazi uliofanyika katika ukumbi wa Makumbusho ya Taifa jijini Dar es salaam.
Afisa Elimu Makumbusho ya Taifa Tanzania, Bi Anamery Bagenyi akifafanua jambo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) mara baada ya ufunguzi wa mkutano wa vijana  kujadili ushirikishwaji wa vijana kuhusu masuala ya afya ya uzazi uliofanyika katika ukumbi wa Makumbusho ya Taifa jijini Dar es salaam.
mwakilishi kutoka Shirika la Idadi ya Watu la Umoja wa Mataifa (UNFPA)nchini, Dkt. Wilfred Ochan akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) mara baada ya ufunguzi wa mkutano wa vijana  kujadili ushirikishwaji wa vijana kuhusu masuala ya afya ya uzazi uliofanyika katika ukumbi wa Makumbusho ya Taifa jijini Dar es salaam.
 

Dar es Salaam:

ASASI ya Vijana ya Umoja wa Mataifa (YUNA Tanzania) imeandaa kufanya kongamano kubwa la kimataifa litakalofanyika mapema mwezi huu mkoani Morogoro na kuwakutanisha vijana kutoka mataifa mbalimbali dunia.

Akizungumza jijini Dar es Salaam na Mwenyekiti wa YUNA Tanzania, Hortancia Nuhu katika mkutano walioandaliwa kwa vijana na wadau mbalimbali kwa lengo la kujadili ushirikishwaji wa vijana kuhusu masuala ya afya ya uzazi uliofanyika katika ukumbi wa Makumbusho ya Taifa.

“Tupo hapa kama vijana wa YUNA, tumeshiriki katika mkutano huu ambao ni moja ya mikutano wa utangulizi kuelekea kongamano kubwa litakalofanyika mwezi huu mkoani Morogoro, huu ni mwanzo wa kile ambacho tunaemda kukifanya Morogoro,” alisema Nuhu.

Alisema moja ya mada ambazo zitajadiliwa katika mkutano huo mwaka huu ni ushirikishwaji wa vijana katika masuala ya afya ya uzazi namna ya kuzuia ukatili wa kijinsia katika masuala mazima ya mahusiano.

Nuhu aliongeza kuwa wameona kabla ya mkutano huo mkubwa wakutane na wadau mbalimbali ili kupata maoni yao kujua mambo mbalimbali kuhusu ushirikishwaji wa vijana katika masuala ya afya ya uzazi.

“Hii itatusaidia hata tutakapofika katika mkutano wa mwezi wa tano, tuweze kujua kwamba mashirika gani tulishirikiana nayo katika kupata suluhisho juu ya hii mada inayohusiana na masuala ya uzazi kwa vijana,” ameongeza Nuhu.

Nae Afisa Elimu Makumbusho ya Taifa Tanzania, Bi Anamery Bagenyi amesema leo tuna mkutano wa vijana mkutano ambao unawakutanisha vijana kutoka vyuo vikuu na taasisi mbalimbali za elimu ya juu vilivyopo vilivyopo Dar es Salaam kwa lengo la kuwaleta pamoja vijana kujadili masuala yanayowahusu.

“Ninaposema masuala yanayotuhusu, ninamanisha kuna masula ya kijamii ambayo tuna kutana nayo, kuna masuala ya mahusiano ambayo vijana tunakutana nayo na pangine mtu anashindwa hili nianzie wapi,”.

Kupitia mkutano huu vijana watajadiliana mambo wanayokutana nayo na kujua namna ya kukabiliana nayo hususan changamoto zinazotokana na mahusiano.

Akizungumzia ushiriki wa Makumbusho ya Taifa katika mkutano huo bi. Bagenyi alisema Makumbusho ni sehemu kwa ajili ya kila mtu wakiwemo vijana.

“Na tumekuwa na jukwaa linalojulikana kama Museum University House. Kupitia jukwaa hili tumekuwa tukiwaleta wanafunzi wa vyuo vikuu pamoja ili kujadili changamoto na fursa ambazo zinapatikana baada ya kuwa wamehitimu,” amesema.

Kwamba kupitia jukwaa hili vijana wamekuwa wakijadili wapi wanaweza kupata ajira baada ya kuhitimu masomo yao.

Aidha kwa kuwa Makubusho ya Taifa ni kivutio cha utalii, ametumia fursa hiyo kuwaalika vijana kufika kujifunza na kuona uzuri wa Tanzania.

Kwa upande wake mwakilishi kutoka Shirika la Idadi ya Watu la Umoja wa Mataifa (UNFPA)nchini, Dkt. Wilfred Ochan alisema ameshiriki mkutano huo kuonesha ushirikiano kwa waandaaji ambao ni YUNA Tanzania.

"Mkutano huu pia umejikita kujadili majukuma ya vijana katika afya ya uzazi. Hivyo ninapenda kusikia maoni na ushauri kuhusu hili,” amesema Ochan.