ZUNGU AFUNGA MAONESHO YA WIKI YA MACHINGA COMPLEX
Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, mhe Mussa Zungu akizungumza katika ufungaji wa wiki ya maonyesho ya biashara ya wafanyabiashara wa Soko la Machinga Complex Ilala jijini Dar es Salaam.
NAIBU Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, mhe Mussa Zungu akikagua. Mabanda ya wafanyabiashara katika ufungaji wa wiki ya maonyesho ya biashara ya wafanyabiashara wa Soko la Machinga Complex Ilala jijini Dar es Salaam.
Wafanyabiashara na washiriki wa wiki ya maonyesho ya biashara ya wafanyabiashara wa Soko la Machinga Complex Ilala jijini Dar es Salaam.
Dar es Salaam:
NAIBU Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, mhe Mussa Zungu amefunga wiki ya maonyesho ya biashara ya wafanyabiashara wa Soko la Machinga Complex lililopo Ilala jijini Dar es Salaam.
Mhe Zungu alimpongeza Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Amos Makala kwa jisnsi alivyowashirikisha wafanyabiashara hao katika kuwapanga kwenye maeneo ya kufanyia shughuli zao.
“Baada ya kupangwa mabenki yatakuja. Hivyo mtumie fursa hii kwa ajili ya kukopa na kukuza biashara zenu. Kwahiyo nampongeza RC Makalla kwa kazi nzuri anayoifanya akishirikiana na ninyi,” amesema Zungu.
Kuhusu deni ambalo linadaiwa Jengo la Machinga Complex, Zungu amesema kuwa jambo hilo linashughulikiwa baina ya NSSF na Jiji la Dar es Salaam ambapo aliwaahidi wafanyabiashara hao kuwa muda sio mrefu taarifa itatolewa.
Hata hivyo amewataka wahusika kuhakikisha wanalishughulikia suala hilo haraka iwezekanavyo na aliwataka wafanyabiashara wa Machinga Complex kutokata tama bali wafanye kazi kwa bidii kwani Serikali Ya Rais Samia Suluhu Hassan inawajali.
Amewaahidi kuwa Serikali itaendelea kuboresha mazingira ili yawe mazuri zaidi kwa ajili ya kurahisisha shughuli zao za biashara.







