Breaking News

BRELA YANDAA WIKI YA HUDUMA KWA WATEJA JIJINI DAR

Na Timothy Marko
Wakala wa usajili wa Makapuni nchini (Brela)imewataka wafanyabishara wa Makapuni kujitokeza katika Viwanja vya Makumbusho kuweza kutoa Changamoto za usajili wa Makapuni yao.

Akizungumza na waandishi wa Habari jijini Dar es  Salaam, Kaimu Mkurugenzi Idara ya Makapuni na    majina ya Biashara Bwana Meinrad Rweimamu amesema kumekuwepo na changamoto nyingi katika baadhi ya Makapuni moja ikiwemo kuongezwa kwa wanahisa kwenye kampuni pasipo kufuata sheria.

"Hii ni fursa Muhimu kwa wafanyabishara na wamiliki wa makampuni kuja hapa Makumbusho ya taifa posta kueleza changamoto mbalimbali wanazokumbana nazo katika kapuni au utekezaji wa kazi zao hili kupatiwa ufumbuzi". Alisema Bw. Rweimamu 

Alisema Rwemamu kampeni hiyo ambayo  inaanza kuanzia tarehe 13 hadi 19 mwaka huu katika viwanja vya makumbusho ya taifa posta. Ni mahususi kwao kuweza kupata majawabu na elimu juu ya mambo mbalimbali yanayotekelezwa na Wakala wa usajili wa Makapuni nchin (Brela).

Aliongeza kuwa kumekuwa kutokana na kuwepo na changamoto ya mambo mbalimbali hususani kuhusu matukio kama pale mwanahisa mmoja akifariki kupelekea kutokea kwa Migogoro kwenye Makapuni.

"lengo ya kuwepo hapa ni pamoja na kuhakikisha tunasikiliza na kutolea ufafanuzi au usuluhishi chongamoto zote za wadau wetu hasa katika Makapuni". Alisisitiza  Rweimamu.