SAKATA LA NGORONGORO, LHRC WATOA TAMKA ZITO
Kituo cha sheria na haki za binadamu Nchini (LHRC) kimetoa wito kwa serikali kutoa taarifa za watu wanaodaiwa kushikiliwa na Jeshi la polisi pia wameitaka mamlaka hiyo kutoa taarifa juu ya wananchi wa Tarafa ya Loliondo ambao hawajulikani walipo.
Katika Taarifa yao walioitoa leo June 12, 2022 kwenye tamko rasmi zililosainiwa na Mkurugezi wa Kituo hicho Anna Henga zimeeleza kuwa mpaka taarifa hiyo ikitolewa madiwani baadhi ya wananchi na Viongozi kutoka ngazi za vijiji na Kata hawajulikani walipo.
Taarifa hiyo imeeleza kuwa endapo zoezi linalofanyika litakuwa na haja, wameshauri kuwa ni vyema likatekelezwa kwa uwazi na kufuata misingi ya sheria bila ukiukwaji wa haki za binadamu.





