SELASINI: TAKUKURU KUFANYENI UCHUNGUZI RIPOTI YA GAC JUU YA UBADHILIFU MALI ZA CHAMA
CHAMA cha NCCR Mageuzi kimeiandikia Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) kufanya uchunguzi na kisha kuwaita na kuwahoji wale wote waliohusika katika ufujaji wa mali za chama hicho na hatua za kisheria zichukuliwe dhidi yao.
Akizungimza na waandishi wa habari makao makuu ya chama hicho jijini Dar es salaam Mwenyekiti wa Baraza la Wadhamini, bwana Joseph Selasini amesema tayali ofisi yake imeshachukua hatua ya kuiandikia barua TAKUKURU juu ya swala hilo.
“Tulikuwa na kikao cha dharura cha Baraza la Wadhamini, na maamuzi tumeiandikia barua TAKUKURU ichukue taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi wa Hesabu za Serikali (CAG) kuhusu chama chetu, kwa Msajili wa Vyama vya Siasa, iwahoji na hatua zichukuliwe dhidi ya Mbatia na wenzake waliohusika,” Alisema Selasini.
Alisema siku chache zilizopita kumekuwepo na taarifa katika mitandao ya kijamii inayoelezea kuwa chama hicho kimeanza kuendeshwa kwa misingi ya udini napenda kuwajulisha kuwa wao kama chama hawahusiki na wala hakuna masuala ya udini kama ambavyo imekuwa ikielezwa katika mitandao ya kijamii na baadhi ya watu ndani ya chama hicho.
Bw Selasini aliongeza kuwa kuna baadhi ya Viongozi ambao wanataka kukiingiza chama hicho kwenye masuala ya udini jambo ambalo ni kinyume ya misingi ya amani ya nchi yetu.
“Hili ni jambo kubwa, hatuwezi kukaa kimya ni jambo linalogawa nchi yetu, hivyo huo sio msimamo wa Chama chetu, aliyesema hayo ni mtu binafsi na ni uchochezi. Naomba vyombo husika vimchukulie hatua,” ameongeza Selasini na kusisitiza.
“Hatuwezi kuligawa Taifa kwa sababu za udini, Mkutano wa Halmashauri Kuu wa Mei 21 Mwaka huu ulikuwa na wajumbe wa pande zote mbili za Muungano. NCCR hatuna hoja za udini. Tunaikataa hoja hiyo ya udini na tunaziomba mamlaka ifike hatua watu kama hawa wanaotishia amani ya nchi washughulikiwe,”.
Hivyo amemtaka aliyekuwa Mwenyekiti wa Chama hicho James Mbatia na kundi lake waache propaganda za kitoto za kuhamasisha udini, ukabila, ukanda, Utanzania Bara na Uzanzibar.




