Breaking News

NANENANE 2022: DKT KIJAZI ASISITIZA WAKULIMA KUSAJILI VITUO VYA HALI YA HEWA

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) na Makamu watatu wa Rais wa Shirika la Hali ya Hewa Duniani, Dkt. Agnes Kijazi amesisitiza wakulima wanaomiliki vifaa vya hali ya hewa kusajili vifaa hivyo kwa kuzingatia taratibu na sheria.

Aliyasema hayo tarehe 4 Agosti 2022 katika banda la TMA kwenye Maonesho ya NaneNane 2022 yanayoendelea Kikanda Mkoani Morogoro.

Sheria ya Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania Na. 2 ya mwaka 2019 inawataka wamiliki wote wa vituo vya hali ya hewa kusajili vituo hivyo kupitia Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania ili kukidhi matakwa ya kisheria.