UWT ILALA WAANDA SEMINA YA SENSA
Na Heri Shaaban (Ilala)
UMOJA wa Wanawake UWT Wilaya ya Ilala wameanda semina Maalum kwa Wanawake wote wa Wilaya ya Ilala kwa ajili ya kuhamasisha kutoa elimu ya sensa ya Watu na Makazi ambayo inatarajia kufanyika Agosti 23 Mwaka huu .
Katibu wa Umoja wa Wanawake UWT Wilaya ya Ilala Angela Masam ,amewataka Wanawake wote kushiriki siku ya Leo kwa ajili ya kupewa Elimu hii muhimu ajili ya kujua umuhimu wa Sensa kwa ajili ya Maendeleo ya Taifa letu na Wilaya ya Ilala kwa ujumla .
"Tumeandaa siku ya semina ya sensa kongamano hili litawakutanisha Wanawake wote wa majimbo matatu Ilala ,Segerea na Ukonga katika ukumbi wa check Point Pugu Agosti 14 kuanzia saa tatu asubuhi " alisema Angela .
Katibu Angela alisema katika semina hiyo ya Sensa ya watu na Makazi kwa Wanawake ya UWT Wilaya ya Ilala itaongozwa na Wabunge wa Viti Maalum Mkoa wa Dar es Salaam Marim Kisangi ,na Stella Ikupa .
"Nawaomba Wanawake wa Wilaya ya Ilala tujitokeze siku hii muhimu tuweze kupewa elimu hii tukaitumie kuwapa wezetu waweze kujua umuhimu wa sensa ya Watu na Makazi pamoja na kuunga mkono juhudi za Rais wetu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suruhu Hassan.




