KENAN ASIMAMISHA JIJI LA DAR.. AZINDUA NYUMBA ZA MAKATIBU WA CCM
Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa CCM Ndg.Kenan Laban Kihongosi amesimamisha jiji la Dar es salaam kwa masaa nane katika ziara yake ya uzinduzi wa nyumba za makatibu katika wilaya za ubungo na Kinondoni.
Katika ziara hiyo iliyoanza kwa kuzindua nyumba za mtumishi katika wilaya ya ubungo na Kinondoni na kumalizika siku ya kesho kwa kuzindua nyumba ya mtumishi wilaya ya Kigamboni
Ndg. Kenan ametumia fursa hiyo kuwashukuru wote waliojitolea mali, nguvu na muda wao katika kuhakikisha kuwa wazo hilo ambalo lilitolewa na baraza Kuu la Umoja wa Vijana wa CCM linatimia hususan vijana wa Hamasa, madiwani, wabunge na wajumbe wa kamati za ujenzi, aidha Ndg. Kenan amewapongeza wabunge madiwani na viongozi wa ngazi zote kwa kushiriki katika shughuli mbalimbali za ujenzi wa Chama na Jumuiya zake.
Akihutubia katika hadhara zote mbili wilayani ubungo na Kinondoni Ndg. Kenan amewataka vijana kuwa imara kutotumika na mtu kwa sababu ya kitu bali kuwekeza nguvu, maarifa na muda katika kukitumikia Chama Cha Mapinduzi jambo ambalo litawafanya kufika mbali kimalengo ndani na nje ya Chama,ً aidha amewaasa vijana kuzilinda tunu za taifa kwa wivu mkubwa kwani hatuna taifa jingine zaidi ya Tanzania.
Akiendelea kusisitiza juu ya kukilinda Chama Cha Mapinduzi sambamba na kumlinda Mwenyekiti na Rais wa Jamhuri Ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa kazi kubwa na nzuri anayoifanya ambayo wanufaika wake wakubwa ni vijana.
Ndg. Kenan yupo katika Mkoa wa Dar es salaam kwa ziara maalum ya uzinduzi wa nyumba za makatibu katika wilaya mbalimbali za Mkoa huo.







