MASHINDANO YA LIGI YA SNIPER’S POOL PRIMIER LEAGUE KUANZA SEPT 23 JIJINI DAR
Dar es salaam.
Mashindano ya ligi ya Pool Table yanayojulikana kama Sniper’s Pool Primier League (SPPL) yanatarajiwa kuanza rasmi Septemba 23 hadi Novemba 23 jijini Dar es salaam.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam na Mratibu wa Shindano hilo, bwana Ashish Cinematography juu ya maandalizi ya shindano hilo amesema lengo la kuandaa ligi hii ni kusaidia kuongeza viwango vya wachezaji wa mchozo huo nchini kuweza kufikia viwango vya kimataifa.
"Leo tupo hapa kwa ajili ya kuwatangazia wadau na wapenzi wa mchezo wa Pool table kuwa mashindano ya ligi ya mchezo huu yanatarajiwa kuanza rasmi 23 septemba hivyo nitoe wadau kujitokeza kushiriki" Alisema bw. Cinematography.
Alisema lengo kubwa la kuandaa ligi hiyo ni kuhakikisha kuwa wanakuza na kutangaza wachezaji wetu kuweza kufikia viwango vya mchezo huo kufikia viwango vya kimataifa Pamoja na kuongeza kipato kwa wachezaji.
Mapema akizungumzia maandalizi ya ligi hiyo Mwenyekiti wa Hamasa Taifa (TAPA) bwana Mathias Mrosso amesema ni Pool Table ni moja kati ya michezo mikubwa nchini kwani umeshailetea sifa na heshima Tanzania Kimataifa.
“Tumeshawahi kuchukua tuzo ya bingwa wa Afrika ambayo tuliichukua mwaka 2013. Kipindi hicho mchezo ulikuwa unachezwa na kupendwa sana,” amesema Mrosso.
Mrosso amesema ligi hii itashirikisha wachezaji bora kitaifa 20 na kwamba mshindi wa kwanza atapata shilingi milioni 1.5, wapili shilingi laki 8 na watatu shilingi 5
Aidha amewata wadau na wapenzi wa mchezo huo kutumia fursa hiyo kujitokeza kwa wingi kushiriki shindano la mwaka huu.
Kwa upande wake Mdhamini wa Ligi hiyo Jeremiah Mayanga kutoka kampuni ya Smile Sasa amesema kazi yao kubwa itakuwa ni kulitangaza shindano katika mitandao ya kijamii ili lifahamike na kukaribisha wadau Zaidi kudhamini.




