Breaking News

HAYA HAPA MATOKEO YA DARASA LA SABA (PSLE 2023)

Baraza la mtihani tanzania (NECTA) wametangaza matokeo ya mtihani wa kumaliza elimu ya msingi uliofanyika September mwaka huu ambapo asilimia 80.58 ya watahiniwa 1.397.293 waliofanya mtihani huo wamefaulu kwa daraja la A, B na C.

Akizungumza jijini Dar es Salaam katibu mtendaji wa  Baraza la mtihani, dokta Said Mohamed alisema matokeo ya mwaka huu yanaonyesha kuwa kiwango cha ufaulu kimeongezeka kwa asilimia 0.96.