Breaking News

MAHAFALI YA 16 YA CHUO CHA KODI KUFANYIKA NOV 24 JIJINI DAR

Mkuu wa Chuo cha kodi (ITA), Profesa Isaya Jairo akifafanua jambo kwa waandishi wa habari juu ya maandalizi ya mahafali ya 16 ya chuo hicho yatakayofanyia 24 mwezi huu jijini Dar es salaam. 

Dar es salaam:
Naibu Waziri wa Fedha, mheshimiwa Hamad Hassan Chande anatarajiwa kuwa Mgeni Rasmi kwenye Mahafali ya 16 ya Chuo Cha Kodi (ITA) yatakayofanyika Novemba 24, 2023 jijini Dar es Salaam.

Kwa kuzingatia uhusiano na ushirikiano wa Chuo Cha Kodi na Mamlaka za Usimamizi wa Kodi Afrika tayari Mamlaka ya Mapato Uganda wamethibtisha kuhudhuria Mahafali hayo. 

Akizungumza na waandishi wa habari jjini Dar es Salaam, Mkuu wa Chuo hicho Profesa Isaya Jairo amesema jumla Wahitimu 508 watahitimu katika ngazi mbalimbali katika mwaka wa masomo 2022/ 2023 Wanaume ni 293 na Wanawake 215.

"Jumla ya wahititimu 508 wanajarajiwa kuhutimu katika ngazi mbalimbali katika mwaka wa masomo 2022 / 2023 ambapo Wanaume ni 293 na Wanawake 215" Al8sema Prof. Jairo. 

Alisema katika mahafali ya mwaka huu Wahitimu watakao tunukiwa cheti cha Uwakala wa forodha na kodi ni 43, Stashahada ya Uwakala wa Usimamizi wa forodha na kodi ni 39, Watakaotunukiwa Stashahada ya juu ya forodha na kodi ni Wanne, Shahada ya forodha na Kodi ni 117, na wahitimu watakao tunukiwa Stashahada ya Uzamili ya kodi kwa mwaka huu ni 52. 

Prof. Jairo, aliongeza kuwa Chuo Cha Kodi kinajivunia mafanikio mengi, lakini katika mpango mkuu wa tano wa chuo ambao umejikita katika kutoa mafunzo kwa njia ya kisasa ya Kidijitali.