WALEZI WALETENI WATOTO KUPATA ELIMU YA UJUZI VETA
Meneja mahusiano wa mamlaka ya elimu na mafunzo ya Ufundi stadi (VETA), Mh. Sitta Petter amewashauri wazazi/walezi na wanafunzi wa kidato cha nne kwa ujumla wake kuanza kufikilia kusoma mafunzo ya ufundi ili kujipatia ujuzi wakati huu ambao wanasubiri matokeo ya kidato cha tano kutoka
Bi Sitta ametoa rai hiyo wakati akizungumza katika Viwanja vya mnazi mmoja ambapo yanafanyika maonesho ya miaka 50 ya Necta.
“Tuna vijana wengi ambao wamemaliza kidato cha nne ambao wanasubiri matokeo kutoka, tunaamini wapo ambao watakwenda kidato cha tano lakini pia wapo watakaokwenda vyuo vya ufundi, tunawaambia wakati huu ambao wapo kipindi cha mpito watumie fursa hii kusoma kozi fupi za ufundi stadi,” alisema bi. Sitta
Amesema badala ya kuwapeleka watoto kusoma masomo kwa ajili ya kidato cha tano (Pre-form five), basi watumie muda huo kujifunza ujuzi, kwani mitaala ya sasa inasukuma Zaidi ufundi
Amesema faida ya kusoma ufundi stadi ni pamoja na kuwa katika nafasi nzuri ya kupata ujuzi ambao utakusaidia katika Maisha yako, kwamba kijana ambaye anao ujuzi anakuwa tofauti na yule ambaye bado hana ujuzi.
Mimi niko form five lakini tayari fundi umeme, au fundi magari, inawezekana kabisa hata wakati wa likizo akirudi anaweza kuendeleza fani yake, jambo hili linawezekana kabisa,” alifafanua
Mtoto anapokwenda kusoma Pre-form five halafu hakubahatika kufaulu maana yake mzazi amekula hasara, lakini mtoto naye amepoteza muda wake, lakini akipata ujuzi atakuwa msaada katika familia,” aliongeza
Aidha bi. Sitta amesisitiza kuwa elimu ya sasa ina mikondo miwili, upo ule wa kawaida lakini pia upo wa mafunzo ya amali, ni vizuri wazazi wakalifahamu hilo na kuandaa Watoto watakaoingia katika makundi hayo




