Breaking News

ACT WAZALENDO KUKUTANA NA RAIS SAMIA, MWINYI KUINUSURU SERIKALI YA UMOJA WA KITAIFA ZANZIBAR

Kamati ya Uongozi Taifa ya chama cha ACT Wazalendo imeazimia kuonana na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Rais wa Zanzibar kuwaeleza juu ya uamuzi wa Chama hicho kujitoa katika Serikali ya Umoja wa Kitaifa kutokana na kushishindwa kutekelezwa kwa makubaliano yaliyoingiwa na Marehemu Maalim Seif Sharif Hamad kwa niaba ya ACT Wazalendo na Rais Mwinyi kabla ya ACT Wazalendo kujiunga na Serikali ya Umoja wa Kitaifa.

Akizungumza na waandishi wa habari, Katibu hicho, Ado Shaibu alisema uamuzi huo ni moja ya maadhimio umefikiwa katika kikao cha Halmashauri Kuu Taifa ya chama hicho iliyokutana Machi 4 mwaka huu makao makuu ya chama hicho, Magomeni jijini Dar es Salaam.

Alisema uwepo wa Serikali ya Umoja wa Kitaifa ndio zao la utulivu wa kiuchumi, Utalii, mikopo na biashara kwani ni roho ya uchumi inayotegemea utulivu.

"Serikali ya Umoja wa Kitaifa ni zao la damu ya Wazanzibar, kwa wote mashahidi karibu kiila uchaguzi watu hufa mfano uchaguzi wa 2020, walifariki watu kutokana na vurugu za uchaguzi," alisema na kuongeza

Mnapozungumzia tamu ya Serikali ya Umoja wa Kitaifa ni damu ya watu, kama halitazamwi jambo hili kwa jicho la pili, ndio maana tunataka kukutana mapema iwezekanavyo na Marais wote wawili.

Shaibu aliongeza kuwa kikao hicho cha Halmashauri Kuu Taifa pia kilifanya tafakuri ya kina juu ya mwenendo na mwelekeo wa Serikali ya Umoja wa Kitaifa Zanzibar.

Alisema uwepo wa Serikali ya Umoja wa Kitaifa ni matakwa kisheria kati ya aliyekuwa kiongozi wa chama hicho, marehemu Maalim Seif Sharif Hamad kwa hoja tatu.

Alizitaja baadhi ya hoja hizo kuwa ni pamoja na kuachiwa huru kwa viongozi wote wa ACT wanaoshikiliwa kwa hila, watuhumiwa hao ni lazima wafidiwe sambamba na mageuzi ya kimfumo na usimamizi wa uchaguzi ukiacha suala la kuachiwa huru kwa wanachama waliokuwa wanashikiliwa kutokana na uchaguzi mkuu 2020, hakuna hoja nyingine kati ya zilizowasilishwa ambayo imefanyiwa kazi na Rais wa Zanzibar Ndugu Hussein Mwinyi.