MUFTI KUONGOZA DUA YA KUMUOMBEA HAYATI MZEE MWINYI 11 MARCH
Samaha Mufti wa Tanzania Abubakar Zubeir Ali Mbwana anawaalika waislamu na waumini wote kuhudhuria Dua kumuombea Rais wa Awamu ya pili Almargoum Ali Hassan Mwinyi
Kwa Mujibu wa Taarifa maalum iliyotolewa na katibu mkuu wa Bakwata Alhaj Nuhu Jabir Mruma dua hiyo itafanyika kesho Saa saba mchana kwenye msikiti wa mfalme Mohammed VI Bakwata Makao Makuu jijini Dar es salaam.
Alhaj Mruma amewataka Viongozi wa taasisi na madhehebu mbalimbali na viongozi wa Bakwata mikoa na wilaya kudhuria na hasa viongozi wote wa Bakwara Dar es salaam wa Ngazi ya mkoa, wilaya zote, kata na maimamu wa jiji la Dar es salaam pamoja na waumini wote.
Alhaj Mruma amesema maandalizi yote yamekamilika na kwamba waumini wote ni vyema wafike mapema ili kujumuika pamoja kuanzia mwanzo wa Dua.




