Breaking News

ATUPWA MIAKA 20 JELA KWA KUHUJUMU MIUNDOMBINU YA TANESCO

Jeshi Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam katika kusimamia mifumo ya kisheria ya haki jinai tarehe 21 Novemba, 2022 mtaa wa Mbozi Temeke lilimkamata Lusekelo Kalinga (47) Mkazi wa Sinza na kumfikisha Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam.

Akielezea tukio hilo kamanda kamanda SACP Muliro Muliro amesema mara baada ya baada ya mashauri yake kusikilizwa tarehe 2 Mei, 2024, mshtakiwa huyo alipatikana na hatia na kupewa adhabu ya kifungo cha miaka 20 jela.

"Mara baada ya mashauri yake kusikilizwa ambapo tarehe 2 Mei 2024, mshtakiwa huyo alipatikana na hatia na kuhukumiwa adhabu ya kifungo cha miaka 20 jela kuhusiana na kosa alilolitenda la kuhujumu miundombinu ya Shirika la umeme TANESCO." Alisema SACP Muliro.

Katika hatua nyingine Jeshi la polisi linawashikilia kwa mahojiano Javani Ochengi (36) Raia wa Kenya, mkazi wa Kimara, Yohana Mroso (20) mkazi wa Mbagala, Fransis Asangwile (34) mkazi wa Kongowe na Auston Mpanju (32) mkazi wa Tuangoma kwa tuhuma za kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu.

Alisema watuhumiwa hao wamekuwa wakijinadi kuwa wao ni wakala wa mafunzo ya biashara, kutafutia vijana shule, vyuo, kazi au sehemu za utalii nje ya nchi kwa kuwahadaa watu walipe pesa kupitia kampuni ijulikanayo kwa jina la PROFFESION EXCHANGE PLATFORM (PEXPLA).

"Watuhumiwa wamekuwa wakiwahadaa watu walipe pesa ili wasaidie kupata nafasi wanazo hitaji kitendo na kukusanya kiasi kikubwa cha pesa toka kwa wananchi kisha kutoweka." Alisema SACP Muliro.