Breaking News

BUKUKU: MATUMIZI SAHIHI YA MITANDAO YA KIJAMII YATAONGEZA TIJA KWA TAIFA

Fursa ya matumizi ya mitandao ya kijamii nchini inaweza kuwa na tija kama itatumika vizuri hususani katika kusaidia jamii kutatua changamoto mbalimbali zinazowakabili.

Akiwasilisha mada katika kongamano la Jumuiya ya wanahabari wa mitandao ya kijamii mmiliki wa mtandao wa Fullshangwe, John bukuku amesema wanahabari wa mitandao tunapaswa kipindi chote cha utendaji kudhingatia sheria miongozo na kanuni. 

"Kama mwanahabari hususani wa mitandao ya kijamii kuna haja ya kutambua na kuzingatia miiko na sheria zote zinazongoza katika utekelezaji wa majukumu yetu kwa lengo la kuhakikisha kuwa tunatoa taarifa ambazo zitakuwa na tokeo chanya kwa taifa na jamii kwa ujumla" Alisema Bw. Bukuku

Alisema Katika kipindi chote wanahabari hasa wa mitandao ya kijamii wajitajidi kujikita zaidi kuripoti matukio chanya kwa jamii kwa lengo la kujiongezea uaminifu kwa jamii pamoja na taasisi mbalimbali.