DUKA LA KISASA LA SIMU MANDASI STORE LAFUNGULIWA JIJINI DAR
Mstahiki Meya wa Jiji la Dar es salaam Omary Kumbilamoto akipewa maelezo kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Mandasi Store, Abdullahi Mandasi juu bidhaa na ubora wake mara baada ya ufunguzi wa duka hilo la kisasa la Mandasi Store lililopo banana jijini Dar es salama.
Mstahiki Meya wa Jiji la Dar es salaam Omary Kumbilamoto akizungumza katika uzinduzi wa duka la kisasa la simu la Mandasi Store lililopo banana jijini Dar es salama
Balozi wa duka la kisasa la Mandasi Store, Dotto magari akimwelezea jambo Mstahiki Meya wa Jiji la Dar es salaam Omary Kumbilamoto juuya bidhaa mbalimbali zinazopatikana katika uzinduzi wa duka la kisasa la simu la Mandasi Store lililopo banana jijini Dar es salama
Dar es salaam.
Mstahiki Meya wa Jiji la Dar es salaam Omary Kumbilamoto amewataka wananchi wa jiji hususani Banana na maeneo jirani wanaokopa simu katika maduka kuwa waaminifu kwa kulipa mikopo yao na sio kutafuta njia kukwepa mikopo ili kuhakikisha huduma hiyo inawafikia wengi zaidi.
Wito huo ameutoa mapema leo jijini Dar es salaam wakati akizindua Duka kubwa la Kisasa la Simu, vishikwambi na laptop linalojulikana kama Mandasi Store lilipo maeneo ya Banana jijini Dar es salaam.
Alisema kufunguliwa kwa duka hilo ni hatua ya kupongezwa kwani pamoja na kusogeza huduma karibu na kuuza bidhaa kwa bei nafuu hili watu wengi waweze kuzimudu.
"Mara nyingi Nimekuwa nikialikwa kufungua maduka hasa ya kuuuza simu lakini mengi yamekuwa wamekuwa yakiuza bidhaa zao kwa gharama kubwa ukilinganisha na duka hili la mandasi Store, nimekuta simu orginal kwa bei ya kawaida na kama mteja hana hela taslimu anaweza kukopa na kulipa kidogo kidogo" Alisema Mstahiki Meya Kumbilamoto.
Awali akimkaribisha mgeni rasmi Mkurugenzi Mtendaji wa Mandasi Store, Abdullahi Mandasi alisema tangu kuanza rasmi kutoa huduma nchi wameshatoa mikopo ya simu zaidi ya elfu 26,000 ambapo wanamaduka 14 ndani ya mikoa 10.
Alisema kupitia matawi yao nchinnzima wametoa ajira kwa vijana zaidi ya 36 ambapo pia wameahidi kuendelea kutoa ajira kwa kufungua maduka zaidi katika maeneo mbalimbali.
Akizungumzia ubora wa bodhaa zao pamoja na bei amesema Kuna simu janja zinazoanzia laki moja hadi milioni tatu kiwango cha juu ambazo mteja naweza kuzipata kwa kigezo cha kuwa mtumishi umma ili kurahishia ufuatiliaji wake.
Kwa upande wake balozi wa duka hilo, Dotto magari, amewapongeza Mandasi store kwa kuwa na huduma za maduka nchini ambapo wanatoa ajila kwa vijana pia wanatoa huduma za kuuza simu na mikopo Ambapo inawawezesha watu wakipato cha chini na cha kawaida kupata simu na kulipa kidogo kidogo.








